Wednesday, June 30, 2010

DADA WAWILI MWANAUME MMOJA.............



dada wawili waliozaliwa tumbo moja wamejikuta kwenye kasheske kubwa baada ya kugundua wanachukuliwa na mwanaume mmoja ilikuwa je?
Rhoda na Rachael ni mtu na dada yake, rhoda akapata mwanaume wa maana mwenye kungaramia kwa kila kitu na alikuwa na pesa sana rhoda alichanganyikiwa kwa mapenzi anayoyapata kwa huyu mwanaume kwani walipendana sana..
lakini rhoda hakumuamini huyu mwanaume kama kweli anampenda kiukweli kutoka moyoni basi akapanga na dada yake (mtoto wa mama mdogo ambaye huyu mwanamke wake rhoda hajawahi kumuona) kwamba rachael ajipendekeze kwa yule mwanaume na kuona kama jamaa atamkubali ama atamkataa kwakuwa mwaminifu kwa rhoda...
dada kaingia mchezoni kumjaribu mwanaume maana alishaonyeshwa na namba ya simu akapewa, kwa muda yule kaka bwana kwa vituko vya rachael vya kujipendekeza akakuta kaingia mkenge na sio kiutoto yani mapenzi ya rachael yakamchanganya ile mbaya.......
ikafika wakati akapunguza na baadae akakata mapenzi kwa rhoda, akamuanzia visa kwasababu alishakolezwa na dada mtu,rhoda kugundua mwanaume kakolezwa na dada yake ikabidi amuendee kumuomba msamaha jamaa na kumuhadithia kila kitu, kwani naye rachael amekataa kabisa kuachana na yule kaka........
kwa maajabu jamaa hakushangaa sana na alichokifanya nikuhama nchi na rachael wakaenda kukaa ghana, ambako alikuwa ametokea yule kaka, rhoda akakata undugu na rachael kabisa kwa kisa cha kumchukulia bwana......
kwa niaba ya wanawake wanopenda kuchokonoa wanaume zao kutaka kujuwa kama wanawapenda ama la, wakati mwengine utaujuwa ukweli na wakati mwengine utaharibu uhusiano cha muhimu mpo pamoja basi amini anakupenda na usitafute mengine...
Pole sana rhoda

2 comments:

  1. Huyo Rhoda (pamoja na wanawake au hata na wanaume wenye tabia za kuchokonoana hivyo) alipata alichokihitaji. Inakuwaje umfanyie majaribio mtu umpendaye? Hata kwa wale wakristo watakumbuka katika ile sala yetu maalum huwa tunasali hivi, ....asitutie majaribuni. Siyo vizuri kujaribiana. Kwa kuwa huwezi kujua kiwango cha ustahimilivu wa mwenzio katika majaribu basi unatakiwa umlinde kwa kadri uwezavyo, njia moja wapo ya kumlinda mwenizo ni kumweka mbali na vishawishi au majaribu. Mpe pole sana huyo rhoda, akimpata mwingine hatamchezea. Obazega!

    ReplyDelete
  2. Pole dada rhoda chukulia hilo kama somo na jipe moyo kila likuepukalo lina kheri na wewe

    ReplyDelete