Monday, June 21, 2010

CHUCHU KUBWA.....

Rosemary Mizizi, nimejifungua mtoto wangu wa kwanza siku za karibuni natamani kweli ningeweza kumnyonyesha mtoto wangu lakini nashindwa kutokana na chuchu zangu kuwa kubwa sana kumfanya mtoto ashindwe kunyonya vizuri, nimejaribu kumkamulia maziwa yangu lakini hayatoki ya kumtosha yeye kushiba kwahiyo inabisi nimpe maziwa ya kopo.
nimeambiwa sio vizuri kwa afya mtoto kunywa maziwa ya kopo sasa nitafanyaje na yangu hayatoki mengi hata nikitumia breast pump?
wamama nisaidieni tafadhali

4 comments:

  1. Hongera Rose Mary,

    Rose mimi nilipojifungua mtoto wa kwanza niliambiwa na wifi yangu kuwa ninachuchu kubwa kwahiyo siwezi kumnyonyesha mtoto, kwa hiyo sikumnyonyesha baada ya mwezi mzima, nikawa ninamkamulia na kumpa maziwa ya kopo.Lakini siku kubali ikabili niende kwa mama yangu mzazi (alinionyesha ni jinsi gani ninapaswa kumshika mtoto na kumyonyesha kumbe nilikuwa ninakose jinsi ya kumweka ili apate ziwa baada ya hapo mtoto alizoea nikamshonyesha mpaka miaka miwili na wapili nilimnyonyesha bila wasi wasi.

    Hakuna chuchu kubwa mtoto akinyonya kwa wiki tuu zinachongeka.
    Pia kiliniki zingine uwa wanafundisha wajawazito kuzifinyanga chuchu ili zichongoke wakati ukijifungua zinakuwa na ncha.

    Pia niliambiwa na dada mmoja Agha Khan wanakuwaga na nursury ya wiki kwa wazazi kuwafundisha ni jinsi gani wanapaswa kumshika mtoto.

    REgards,
    gk

    ReplyDelete
  2. endelea kumkamulia kidogokidogo hivyo hivyo anayahitaji ni muhimu sana hasa kwa ukuaji na kumkinga na maradhi madogo madogo

    ReplyDelete
  3. endelea kumkamulia ,hakikisha unakamua dakika kama 15 kila mtoto napomaliza kunyonya , kunywa maji mengi kama glasi kumi kwa siku usichoke , tafuta muda wa kupumzika ,kuna mmea unaitwa fungreek ila kwemye maduka ya vitamins unaweza pata vidonge vyake au maduka ya waihindi ipo ya unga tumia kam akiungo kwenye mboga inaongeza sana maziwa mimi nakamua napata kama oz 9 kwa mkamuo mmoja kwa hiyo nina akiba ya kutosha mengine nagandisha kwenye deep freezer yanakaa mpaka miezi sita bila kuharibika . mimi niliokolewa na website moja inaitwa childcentre ingia na usome kunaushauri mzuri sana na inawezekana mwanangu sasa naumri wa miezi sita na sijawahi mpa ya kopo .

    ReplyDelete
  4. JHHJJGJJJKJKFGJKGJKKGG

    ReplyDelete