Thursday, November 13, 2014

Nampenda sana mke anayejitambua...

KATIKA NDOA YAKE NI MIEZI MIWILI TU YA MWANZO ALIPATA AMANI NA KUMFURAHIA MUMEWE

BAADAE MUMEWE AKABADILIKA SANA MPAKA KUACHA HATA KUMUHUDUMIA MKEWE, HATA HELA YA KULA NYUMBANI AKAWA HAACHI

YULE DADA AKAWA ANAVUMILIA, AKAANZA KUKONDA IKAFIKA WAKATI SASA MUMEWE HALALI NDANI NDIPO YULE DADA KUAMUA KWENDA KWA BABA MKWE WAKI KUMSHTAKIA MUMEWE

BABA MKWE WAKE AKAMSEMA KWELI MWANAE NA KUMSHAURI KWANINI ANAMTESA MTOTO WA WATU MPAKA KUKONDA HIVYO, NA KUMWAMBIA YULE MAMA KWAMBA KAMA MUMEO HAKUACHII HELA UWE UNAKUJA NYUMBANI KULA KWANZIA ASUBUHI MPAKA JIONI UZURI NI KWAMBA HAWAKAI NA NYUMBANI KWA BABA MKWE MAANA MAMA MKWE ALISHAFARIKI

BASI YULE DADA AKAWA ANAENDA KULA KWA BABA MKWE, HUKU MWANAUME HANA HATA TIME NA MKEWE HAMTUNZI WALA HAONEKANIKI NYUMBANI

IKAENDELEA HIVYO KWA MIAKA MIWILI MPAKA WADOGO WA YULE MUME WAKAANZA KUMSHAURI YULE DADA BORA AOMBE TALAKA TU AONDOKE MAANA HAPO ANATESEKA BILA SABABU NA KUONEWA TU NA MUMEWE..YANI ILIFIKIA MPAKA NDUGU WA MUME KUA UPANDE WA MWANAMKE

YULE DADA WA WATU AKACHAKAA KWASABABU YA SHIDA, IKAFIKIA MPAKA MUMEWE SASA HAMGUSI YANI WAKAKAA MWAKA MZIMA KAMA KAKA NA DADA MWANAUME AKIRUDI MAUSIKU ANALALA TU KAMA YUPO KWA MAMA YAKE

SHIDA NA MATESO YALIENDELEA KWA MUDA MREFU SANA, SIKU YULE MAMA AKACHOKA KATIKA PITAPITA ZAKE HUKO AKAKUTANA NA MKAKA MMOJA AMBAYE WAKAWA MARAFIKI

KUTOKANA NA TABU ALIZOKUA ANAPATA YULE MWANAUME NDIO AKAANZA KUMSAIDIA HELA NA KUMTUNZA YULE MWANAMKE YANI YULE DADA AKAAMUA KUCHEPUKA RASMI, NA UKIANGALIA MWANAUME MWENYEWE ANAHELA ANAJIWEZA GARI NA NYUMBA NZURI BASI DADA AKAONA HAPA KAPATA AMANI

MAISHA YAKAENDELEA DADA AKIPENDEZA HUKU ANATUNZWA NA MCHEPUKO, WATU WAKAANZA KUSHANGAA NA KUMUULIZA AKAWA TU ANAWAJIBU NIMEZOEA SHIDA NDIO MAANA NANENEPA NA KUPENDEZA

MUMEWE SASA KUMUONA MKEWE ANAPENDEZA AKAANZA KUWA ANAJIRUDISHA NYUMBANI, JAPO HAWAKUTANI KIMWILI WALA HAKUNA MAPENZI BASI TU AKAANZA KUSHINDA NYUMBANI MARA AKAANZA MTINDO WA KUANGALIA SIMU ZA MKEWE BAHATI NZURI HATA SIKU MOJA HAKUWAHI KUONA MESSAGE ZA YULE BWANA WALA SIMU

MPAKA SIKU HIYO YULE DADA ALIPOCHOKA ALIPOONA KAMA KAWAIDA YAKE MUMEWE KACHUKUA SIMU YAKE AKATOKA NJE NA KWENDA KWA JIRANI RAFIKI YAKE NA KUMUOMBA SIMU YAKE ATUMIE AKACHUKUA NA KUMPIGIA MCHEPUKO NA KUMWAMBIA MUMEWE KASHIKA SIMU YAKE AIPIGE NA KUONGEA NAE AMUULIZIE SASA YULE DADA

KWAKUA MWANAUME ALISHAJUA MAISHA YAO YOTE HAKUONA TABU NA KWAKU ALIMPENDA YULE MWANAMKE ALIKUA TAYARI KWA CHOCHOTE NA LOLOTE LITAKALOTOKEA, BASI AKAIPIGA ILE SIMU NA KWELI AKAIPOKEA MUMEWE

HALLO, NAOMBA KUONGEA NA MWENYE SIMU SAUTI YA KIUME, NAONA MUMEWE MOYO UKAMPASUKA AKAMWAMBIA MWENYE SIMU NI MIMI AKAMWAMBIA SIO WEWE MWAMBIE MWENYE SIMU NIPO NJIANI NAKUJA KAMA TULIVYOKUBALIANA NITAPAKI HAPO NJE KWENYE DUKA LILE LA MBELE, YULE BABA AKAMWAMBIA SAWA

WAKAWASILIANA KUPITIA SIMU YA YULE RAFIKI YAKE KULE NJE KWAMBA YOTE ALIYOMUELEZA MUMEWE NA KWAMBA YUPO NJIANI ANAKUJA LEO LIWALO NA LIWE, MKE NAYE SIJUI ALIPATA WAPI UJASIRI NAYE AKAKUBALI SAWA LIWALO NA LIWE LEO

BASI MCHEPUKO AKAFIKA HAPO DUKANI KAMA WALIVYOKUBALIANA, SASA KULE MUMEWE WALA HAKUMUELEZA MIKEWE KAMA SIMU ILIPIGWA NA MWANAUME KASEMA HIVI NA HIVI KWA AKILI YAKE ALITAKA HUYO KAKA AFIKE AKAMFUNDISHE ADABU SI ALIJIUA NI MWANAUME TU KAMA YEYE

BASI MCHEPUKO ULIVYOFIKA AKAPAKI HAPO DUKANI NA KUPIGA SIMU YA YULE DADA AMBAYO ANAYO MUMEWE KWAMBA NIMEFIKA NIPO HAPA DUKANI, YULE BABA AKATOKA NJE KWA MBELE KUANGALIA AKAKUTA BONGE LA GARI LIMEPAKI RAV 4 MPYA KWANZA AKACHOKA KABISA AKAMTUMA KIJANA NENDA KWENYE ILE GARI MWAMBIE HUYO MTU AJE HUKU, KIJANA AKAENDA

HAPA NDIPO HATA MIMI MWENYEWE NILIYEHADITHIWA NILIVYOCHOKA YANI MCHEPUKO ALIJIAMINI KABISA KUTOKA KWENYE GARI NA KWENDA KUKUTANA NA MUME WA MWANAMKE WAKE LIVE BILA CHENGA, HIVI ALIJIAMINI NINI ANGEULIWA JE, AU KWAVILE MWANAMKE ALISHAMUAMINISHA NDIO MAANA

BASI KUFIKA PALE MKAKA MTANASHATI ALIYEPENDEZA HATARI ANANUKIA BALAA YANI UKIMUANGALIA UNAJUA KABISA HUYU MWANAUME KAOGA NA SIO MUMEWE ANAYESHINDA NA KANZU MUDA WOTE AKAMSALIMIA NA KUMWAMBIA NIMEKUJA KUMUULIZIA MPENZI WANGU MWENYE ILE SIMU NILIYOKUPIGIA

YULE BABA NDIO KUANZA UGOMVI MPENZI WAKO KWANI HUJUI KAMA HUYO MKE WA MTU AKAMWAMBIA MIMI HAKUWAHI KUNIAMBIA KWAMBA ANA MUME NDIO KWANZA NASIKIA LEO BASI IKAWA UGOMVI NA GUMZO WATU NDIO KUINGILIA TENA PALE NA KUAMULIWA AKAITWE MKEWE

MKEWE AKAJA AKAMSALIMIA MCHEPUKO NA ALIPOULIZWA MWANAMKE MWENYEWE NDIO HUYU AKAJIBU NDIO HUYO AKAULIZWA WEWE SI MKE WA MTU KWANINI UNAHAWARA AKAJIBU MIMI SIO MKE WA MTU HUYU ANAYEJIITA MUMEWANGU HAJALALA NA MIMI MWAKA SASA NA DINI INASEMA USIPOLALA NA MKE WAKO NDANI YA MIEZI SITA NIKAMA UMEMPA TALAKA SIO MKEO TENA

NDIO MAANA NIKATAFUTA MWANAUME MWENGINE HAPA NATAKA TU HUYU MUME WANGU ANIPE TALAKA YANGU NIONDOKE NIKAOLEWE NA HUYU ANAYENIPENDA NA KUNITHAMINI

 BASI GUMZO PALE, WAKAACHA BALAAA, MANENO NA AIBU NDUGU WOTE WA MUME WAKAWA UPANDE WA MWANAMKE NA KUKUBALIANA APEWE TALAKA MAANA ALITESEKA SANA

AKAANDIKIWA TALAKA MBILI NA MWANZO ALISHAPEWAGA MOJA MWANAUME ALIPOMUACHA NDANI PEKE YAKE KWAHIYO ZIKAWA TATU KAACHIKA RASMI

TSASA HIVI YUPO EDA YA KUMALIZA MIEZI MITATU ILI AACHIKE RASMI, MUMEWE KAANZA KUJIBEMEBELESHA KWA MKEWE KWAMBA SIONDOKE ABAKI LAKINI MKE HATAKI KUSIKIA

NDUGU WA MUME WANAMWAMBIA KWAMBA AKIOLEWA WASIACHE KUWAALIKA KWANI NI BADO WIFI NA SHEMEJI YAO HAKUA NA KOSA BALI MUMEWE NDIYE MWENYE MATATIZO NA WANAMPENDA

***END****

Reactions:

1 comments: