Sunday, October 19, 2014

Tenga muda ni muhimu...

  TUNAPENDA SANA KUWA NA WATOTO NA FAMILIA KUBWA, LAKINI UMESHAWAHI KUGUNDUA KWAMBA MAMA WEWE NDIO YOU ARE ALWAYS ON THE MOVE MAMBO YAKAWE SAWA NYUMBANI


TUANZE NA HUYU MAMA ASIYEFANYA KAZI MAANA NAJUA WENGINE WETU HUMU NI MAMA WA NYUMBANI HATUFANYI KAZI, NA UNAWATOTO UNAAMKA ASUBUHU UANZA KUANDAA WATOTO WAOGE, UWAPIKIE CHAI, UWAANDALIE NGUO ZA SHULE, WAKATI WANAVAA BABA NAE KAAMKA UMTENGEE MAJI, UKAMNYOOSHEE NGUO, UMPE CHAI MARA HAO WAMEONDOKA KWENDA KAZINI NA SHULE, UANZE USAFI WA NYUMBA, MARA MCHANA HUU HAPA UANZE KUPIKA CHA MCHANA WATOTO WANARUDI WANAKULA UANZE KUSOSHA VYOMBO NA KUHAKIKISHA WANAFANYA HOMEWORK MARA JIONI HII HAPA UANZE KUPIKA CHA USIKU, BABA HUYU KARUDI WALE CHAKULA, UFANYE USAFI BAADA YA KULA, MARA KWENDA KULALA KULE NAPO BABA ANATAKA CHA USIKU UMEPE YANI MPAKA UKILALA MGONGO WOTE UMEKUFA GANZI KWA KAZI NA HAYA NDIO MAISHA YAKO MARA KWA MARA UKIPUMZIKA LABDA SIKU HIYO BABA HAJAKUOMBA CHA USIKU

TUJE KWA MAMA ANAYEFANYA KAZI UNAAMKA SAA KUMI NA MOJA UANZE KUHAKIKISHA DADA KAMA UNAYE AAMKE MUANDAE VITU VYA WATOTO, CHAI NA MENGINEYO HALAFU SAA KUMI NA MBILI UNAANZA KUONDOKA KWENDA KAZINI BORA UWE NA GARI KAMA HAUNA NDIO UNATEMBEA MPAKA KITUONI, UKIFIKA HOI UPANDE GARI MARA FOLENI MPAKA KAZINI, UKUTANE NA BOSS SIKU HIYO ANAKISIRANI BASI KAZI HAZIFANYIKI KWA AMANI MARA SAA KUMI NA MOJA HII, UTEMBEE KUPANDA BUS MPAKA KUFIKA NYUMBANI SAA MBILI AU TATU, NYUMBANI HATA HAMU YA KULA HUNA UNAOGA NA KUTAKA KULALA BABA NAYE ANAKUDAKA MBONA HUJAANGALIA HOMEWORKS ZA WATOTO KAMA HAWAJALALA UANZE KUFANYA NAO HOMEWORK, ILE UNATAKA KULALA SAA NNE NA NUSU BABA NAYE ANATAKA CHA USIKU..MMHH

TUJE KWA HUYU AMBAYE HANA MSICHANA WA KAZI SASA UNAAMKA ASUBUHI, KAMA UNAWATOTO TENA WADOGO NA WANAENDA SHULE UANZE KUWAANDALIA NGUO, CHAI NA MAJI YA KUOGA, KUWAAMSHA TU NI SHUGHULI WAAMKE WAOGE WAANZE KUNYWA CHAI UNAONGEA LISAA LIZIMA WATOTO WANASINZI HUKU WANAKUNYWA CHAI, KAMA WANAJIWEZA NDIO HUKU WANAKUNYWA CHAI WEWE UNAANDAA NGUO ZA BABA UKIMALIZA UNAANZA USAFI LABDA WATOTO WANAONDOKA NA SCHOOL BUS AU NA BABA NDIO UMALIZE USAFI UJIANDAE NA WEWE SASA BORA UWE NA GARI KULIKO KUANZA KWENDA KWENYE KITUO CHA BUS, NJIANI TU MPAKA UFIKE HILO FOLENI USHASINZIA MARA MBILI UFIKE TENA KAZINI MGONO WOTE UNAUMA UTUMIE KAZI UKITOKA SAA KUMI NA MOJA TENA HOI MPAKA NYUMBANI UKIFIKA NI KUPIKA MPAKA MLE SAA TATU NA USIKU BABA ANATAKA KAZI IPO PALEPALE

YANI KWA UJUMLA UWE NA MSICHANA USIWE NA MSICHANA, UWE NA WATOTO USIWE NA WATOTO JUKUMU LA KUITUMIKIA NYUMBA NI YAKO WEWE MAMA

AT THE END OF THE DAY UCHOVU NA UCHOVU NA UCHOVU UNALIMBIKIZANA MWILI UNACHOKA UNAANZA KUUMWA KILA MARA MAGONJWA HAYAISHI, MAPENZI NDANI YANAPUNGUA MAANA HUWEZI KUMPA BABA HAKI YAKE VIZURI UNAJIKUTAA UNALALA TUUU BABA AMALIZE UGEUKE UPANDE WA PILI ULALE USIONEKANE UNAMNYIMA ASIJE TAFUTA SABABU YA KUTAFUTA WANAWAKE WENGINE JE

LAKINI KIUKWELI KAMA SISI WANAWAKE TUNAVYOJUA KUDANGANYA TUMEFIKA KILELENI NDIVYO WANAUME WANAJUA KUDANGANYA WAMEENJOY NA KUFIKA KILELENI, HAIMAANISHI KWAMBA KISA AMETOA SHAHAWA NDIO AMEENJOY SEX NA WEWE HAPANA PALE AMEMALIZA TU HAJA YAKE LAKINI BADO HAJAMALIZA HAMU YAKE, NDIPO ANAPOAMUA KUTOKA SASA NJE KUTAFUTA MTU MWENYE MANJONJO TOFAUTI NA KIFO CHA MENDE

SISEMI KWAMBA KILA MARA AKITAKA MUMEO LAZIMA UWE ACTIVE HAPANA KUNA KUCHOKA JAMANI HATA UWE ACTIVE VIPI MTU WA PILI LAZIMA ATASENSE UNAMDANGANYA, UKICHOKA LALA KIFO CHA MENDE LAKINI SIO KILA SIKU.. NA HAPA MAPENZI NDIPO YANAPOANZA KUPUNGUA BABA NAYE HEKAHEKA ZA KITANDANI ZINAANZA KUPUNGUA KWAKUA HAPATI MUAMKO KUTOKA KWAKO NDIO MAANA MARA NYINGI ANAKUPA KIMOJA TU NA YEYE ANALALA MPAKA ASUBUHI NA ANAWEZA ASIKUOMBE TENA MPAKA BAADA YA WIKI MBILI, MAANA ANAJUA HAKUNA MUAMKO KWANINI AHANGAIKE LABDA KAMA HAJA IMEMSHIKA SANA

NA KUNAKIPINDI BABA ATAANZA KULAUMU WAZI KWAMBA ANABOREKA NA NDOA YAKE KWAMBA HUNA MUDA NAYE, HUNA MUDA NA PENZI KWA UBINAFSI WAO HATA HAONI KAMA MKE KAZI ZOTE UNAZOFANYA NYUMBANI LABDA ANAHISI NYUMBA INAKUA SAWA AUTOMATICALLY KWAHIYO WEWE UNAFANYA MAKUSUDI KUTOKUA NAYE KARIBU, MTOTO AKIFAULU VIZURI ANAJISIFU YEYE ANASAHAU ULE MUDA ULIOKUA UNATOKA KAZINI UMECHOKA LAKINI BADO ULIHAKIKISHA UNAKAGUA MADAFTARI YA MTOTO, AKINENEPA ANAJISIFIA ANASAHU ULE MUDA UNAOAMKA ASUBUHI SANA KUMUANDALIA CHAI NA KUHAKIKISHA USIKU NAKULA BILA KULALA, NYUMBA IKIPENDEZA ANASAHAU WAKATI WOTE UNAOJINYIMA HATA KUNUNUA NGUO MPYA LAKINI NYUMBA YAKO IPENDEZE KWAKUA WEWE NI MAMA..

UTAMKUTA MWANAMKE MDOGO TU MIAKA 25-29 AMEOLEWA KWAKUA MAJUKUMU YAMEKUA MENGI SANA KWAKE UKIMUANGALIA TU KWA MTAZAMO WA NJE UTASEMA ANAMIAKA 35 YANI ALIVYOCHOKA, UMENENEPA KWA KULA SANA KWASABABU YA STRESS UNAONA COMFORT YAKO UPATE KWENYE KULA, SURA IMESHUKA MASHAVU YAMETEPETA HATA MAKEUP HUIJUI, NYWELE NDIO HUJUI WEAVING WALA DAWA YA BOX, KUCHA HUJAWAHI HATA PAKA RANGI, MARAFIKI HUNA YANI UNAITUMIKIA NDOA MPAKA INAKUA DHAMBI NA ADHABU NA SIO BARAKA TENA

MUME NAYE AKIKUONA HIVI ANAKUONA HUFAI, HATAKI TENA KUA NA WEWE KARIBU HATA KWENDA BAR YA JIRANI KUKUNUNULIA SODA TU HATAKI MAANA JAMANI KUSPEND NA MUMEO HATA DAKIKA MBILI MKIWA WAWILI TU NI FARAJA YA AJABU HATA KAMA HANA HELA AKUNUNULIE HATA FANTA TU MKAKAA MKAONGELEA MAMBO YENU, NA MAPENZI YENU YANI UNAPATA NGUVU MPYA YA KUENDELEA NA NDOA

NDIO MAANA WANAWAKE WALIOKWENYE NDOA NIKIONGEA NAO HUWA NAWAAMBIA LAZIMA UTAFUTE MUDA KWENYE NDOA YAKO YA KUA MPENZI, HONEY,BABY, SWEETY, LOVE NA DARLING SIO KILA SIKU YA NDOA YAKO WEWE NI MKE WANGU AU MAMA KHLOE AU WEWE MAMA NANIHII (JINA LA MTOTO WAKO)

NAAMINI KILA MWANAMKE ANA HELA 150,000 HAIKUPIGI CHENGA, UKIITAFUTA UWE NA KAZI AU HUNA KAZI KWA KUACHIWA HELA YA MATUMIZI NYUMBANI, NUNUA HATA KIBUBU UCHANGE HIYO LAKI NA NUSU MARA MOJA KWA MWEZI UWE NA MUDA WAKO WEWE NA MUDA WAKO NA MUMEO, NDIO JIPELEKE SALON KAMA UTASUKA AMA UTARETOUCH NYWELE ZAKO ZIWE SAWA, JIFUNZE KUJIREMBA NENDA KATENGENEZE KUCHA ZAKO PAKA RANGI, NUNUA HATA JEANS MOJA TU NA TOP MPYA, JUMAMOSI MOJA UNAVAA VIZURI UNAJIREMBA VIZURI UNAMCHUKUA HUSBAND LEO TUTOKE MUME WANGU BILL ON ME MNAENDA TU SEHEMU NZURI MNAKAA PAMOJA MNAKULA NA KUENJOY PAMOJA

NA UNAPOKUA HUKO MMEKAA PAMOJA SIO UNAKAA KAMA UNAANDIKA KATIBA YA NCHI, MTOTO WA KIKE UNAKAA KWA MAPOZI KAA KARIBU NA MUMEO UKIONGEA NAYE MUANGALIE USONI KWA MACHO YA MAHABA, MCHEZEE MKONO MKIWA MNAONGEA, MMIMINIE KINYWAJI CHAKE KWENYE GLASS, MKILA MLISHE, ONGEA NAYE JINSI ULIVYOKUA NA HAMU NA YEYE YANI MKIRUDI NYUMBANI LEO UTAMPA RAHA ZA AJABU, AMA KAMA KINA SIYE LIPIA HOTEL MKAMALIZIE USIKU KATIKA HOTEL NA SIO NYUMBANI KUBADILISHA MAZINGIRA..JAMANI THIS IS SO FUN NA MAHABA YATAONGEZEKA MARA KUMI ZAIDI

MUNGU AMEWEKA LILE TENDO LA NDOA KUA TAKATIFU, NA AKALIBARIKI UNAPOLIFANYA UKIWA MTUMWA WA UCHOVU UNAONDOA BARAKA ZAKO LA HILO TENDO UNATAKIWA ULIENJOY HUYO NDIO MUMEO MUNGU AMEKUPA UFANYE NAE HILO TENDO TENA KAMA MIYE NIKIWA NAANDALIWA MOYONI NALISALIA KABISA TUNDA NINALOTAKA KUMPA NA NINALOTAKA KUPOKEA MUNGU AKALIBARIKI TUKAENJOY, NA NALIENJOY SANAAAAA NDIO MAANA NASHANGAA MWANAMKE AKIJA KUNIAMBIA DA ROSE MIMI SIENJOY KABISA TUNDA LA MUME WANGU NASHANGAA KWAKWELI ILA KWA KUWAONGOZA WENGI WAMEANZA KUFURAHIA TUNDA PIA

TUMIKIA NDOA YAKO, LAKINI TAMBUA BARAKA ZAKO KWENYE NDOA, PENDA SANA FAMILIA YAKO NA MUNGU ATAKUBARIKI SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO

***END****

Reactions:

0 comments:

Post a Comment