Thursday, September 25, 2014

Tujifunze kuzungumza na watoto wetu...

NATAKA NIANZIE KWENYE UBEBAJI WA MIMBA, WAKINA MAMA MKISHAJUA MNAMIMBA, UNAIOMBEA MIMBA YAKO??? TOKEA UTUNGWAJI MPAKA, SIKU YA MWISHO?? UNATAMBUA KWAMBA WEWE UNAFANYA TU TENDO LAKINI MUNGU NDIYE ATAKAYEKUPA MTOTO KWA WAKATI WAKE NA WAAINA YAKE ATAKAYE YEYE???

NAJUA WENGI WETU HATATUKUFANYA HIVYO, AU TULIFANYA, NA WENGINE NDIO TUTAANZA LEO, NA WALE AMBAO BADO SIKU UKIBEBA MIMBA UJIFUNZE

WEWE MAMA NDIO WA KUMJENGA MWANAO TOKEA SIKU YA KWANZA MPAKA ATAKAPOFIKA DUNIANI MAISHA ATAKAYOISHI NI MATUNDA YA WEWE MAMA NA NDIO MAANA SIKU ZOTE WATOTO WANAITWA NI WA MAMA

WANAPOANZA KUKUA JAMANI WAKINA MAMA TUWE WA KWELI KWA WATOTO WETU, MAISHA SASA HIVI YAMEBADILIKA SIO KAMA ZAMANI SISI TULIVYOKUA TUNADANGANYWA NA WAZAZI TUNAKUBALI TU MTOTO ALINUNULIWA BASI UNAJUA ALINUNULIWA

ZAMANI WAZAZI WAKO NI WAZAZI WANGU NIKIFANYA KOSA MBELE YAO WALIKUA NA HAKI YA KUNIADHIBU LAKINI SIKU HIZI MTOTO AKIKOSA UKIMUADHIBU MAMA YAKE ANAKUFUNGIA KIBWAYA MPAKA KWAKO, AMA ATAKUAMBIA MWANAE MWACHIE MWENYEWE ANAJUA KUMUADHIBU, KAMA HUJAZAA NDIO UTAAMBIWA UNAMUADHIBU UNAJUA UCHUNGU WA MTOTO WEWE..VISA TU SIKUHIZI

WATOTO SIKU HIZI MIAKA MINNE TU ANAJUA HII NI SIMU ATAICHOKONOA MPAKA AANGALIE VITU HUMO NDANI, WATOTO MIAKA KUMI SIKU HIZI WANASIMU ZAO WENYEWE WAZAZI WANAMPIGIA NA YEYE KUWAPIGIA SIO MBAYA ILA KAMA MZAZI UNAJUA KILICHO KWENYE SIMU ZA WANAO

SIKU HIZI TUNASIKIA SANA WATOTO KULAWITIWA, WATOTO WA KIKE WANAPEWA TU DUDU KAMA KARANGA SIKU HIZI, KWENYE SCHOOL BUS, WAKICHEZA NA MARAFIKI ZAO, AU HATA NDUGU ZETU WA KARIBU NDIO HAOHAO WANATUHARIBIA WATOTO JE KAMA MAMA UMESHAWAHI KUMCHUNGUZA WANAO NA HAPA NI WOTE WAKIKE NA WAKIUME SIKU HIZI WANAFANYIWA HIVI WAKIWA BADO WADOGO

HAWAJUI LABDA KUSEMA, AMA WANAOGOPA BAADA YA KUTISHWA, JE TUMESHAWAHI KUONGEA NAO KWAMBA MTU YOYOTE AKIKUSHIKA HUKU UJE KUNIAMBIA HARAKA, TUMESHAWAHI KUZUNGUMZA NAO HIVI MARA KWA MARA????

WANAPOKUA KWANZIA MIAKA 15 WANAPOVUNJA UNGO JE TUMESHAWAHI KUWAFUNDISHA KWAMBA UKIKUTANA TU NA MWANAUME UTAPATA MIMBA, AMA PEDI ZAKE ANAZOTUMIA AWEKE VIZURI MAANA DAMU ZILE MTU AKIAMUA KUMCHEZEA ANAWEZA MDHURU

JE TUNAONGEA NAO BAADA YA KUVUNJA UNGO KWAMBA UKIKUTANA NA MWANAUME BILA KINGA UTAPA SIO TU MIMBA BALI UKIMWI, JE KAMA WAZAZI TUNAKUA WAKWELI KWA WATOTO WETU JE TUNAONGEA NAO IPASAVYO AMA BADO TUNAWACHUKULIA NI WATOTO TU HAWAWEZI KUJIINGIZA KWENYE MATATIZO

WEWE MAMA ULIYEJIFUNGUA UNAPOMNYONYESHA MWANAO HUWA UNAONGEA NAYE HUKU UKIMUANGALIA USONI KWAMBA HILI ZIWA UNALONYONYA MWANANGU UKAMPENDE SANA MUNGU, UKAWE MTOTO MZURI MWENYE KUTII WAKUBWA, MWENYE HESHIMA, UKAWE KIONGOZI MWEMA JE TUNAONGEAGA NA WATOTO WETU??

JUZI JUMAPILI NILIKUTANA NA RAFIKI YANGU MMOJA AKAWA ANANIHADITHIA MAISHA YAKE KABLA YA KUOLEWA, KWAMBA WAZAZI WAKE WALITENGANA NA YEYE AKAWA ANAISHI NA BABA BAADAE BABA AKAPATA MKE MWENGINE KWAHIYO NYUMBANI KUKAWA NA MAMA YAO WA KAMBO

ANASEMA MPAKA WAZAZI WAKE KUTENGANA ALIKUA NA UMRI WA MIAKA KUMI NA NNE HIVI HATA SIKU MOJA MAMA YAKE HAKUWAHI KUONGEA NAYE KUHUSU WANAUME WALA MIMBA, MIAKA MIWILI BAADAE WAKATI ANAMIAKA KUMI NA SITA AKAKUTANA NA MKAKA KATIKA KUZOEANA SIKU HIYO YULE KAKA AKAMWALIKA KWAKE

YEYE KWA AKILI ZAKE ZA KITOTO AKAJUA NI KUPIGA TU STORY WALIPOFIKA KULE BAADA YA KUPEWA CHIPS MAYAI WAKAJIFUNGIA NDANI YULE KAKA AKAMWAMBIA ANATAKA WALALE YEYE ANASEMA HAKUJUA CHOCHOTE ALIKUA TU ANASHANGAA TULALE MCHANA WOTE HUU LAKINI ALAPUUZIA TU

MARA YULE KAKA NDIO KUANZA KUMVUA NGUO SASA YULE AKAWA KAMA KAPATWA NA MSHANGAO MARA YULE KAKA AKAINGIA NA KUMVUNJA BIKRA YULE DADA ALIPOMALIZA AKAVAA NA KUONDOKA

KURUDI NYUMBANI AKAWA ANASHANGAA DAMU ZINAZIDI TU KUMTOKA BILA KUJUA CHA KUFANYA KWA AKILI ZAKE AKAOGOPA KUMWAMBIA MAMA YAKE WA KAMBO AKAENDA KUONGEA NA DADA WA JIRANI AMBAYE WANAHESHIMIANA NA FAMILIA YAO AKAMWAMBIA TU NATOKA DAMU HUKU LAKINI HAKUMUAMBIA ALILALA NA YULE KAKA YULE DADA AKAMWAMBIA UTAKUA UMEVUNJA UNGO

KIPINDI HICHO KUTUMIA VITAMBAA AKAMPA VITAMBAA BYA KHANGA AKAMKATIA VIZURI AKAMWAMBIA AWE ANAVAA AKIMALIZA AFUE AANIKE CHINI YA KITANDA BASI AKAFANYA HIVYO MPAKA DAMU ILIPOKATIKA

SIKU ZIKAENDA MARA MIEZI MINNE BAADAE AKAANZA KUSIKIA KAMA VITU VIBAMTEMBEA TUMBONI KWA AKILI YAKE YA KITOTO AKAJUA LABDA TUMBO LINAMUUMA AKAWA ANAKUNYWA ASPIRINI KILA MTOTO AKICHEZA ANAKUNYWA ASPIRIN HALAFU TUMBO LINAACHA LAKINI ASIJUE KWAMBA MTOTO HUA ANACHEZA NA KUPUMZIKA

BASI AKAENDELEA HIVYO AKAANZA KUNAWILI NA KUNENEPA SIKU MOJA AKAENDA KUMTEMBELEA MAMA YAKE MZAZI NYUMBANI KWAKE ALIPOFIKA MAMA YAKE AKAMWAMBIA MWANANGU MBONA UMEBASILIKA SANA UMENENEPA HEBU LALA HAPA KITANDANI

NDIO MAMA KUGUNDUA HUYU MTOTO ANA MIMBA ANAKWAMBIA MAMA ALIPIGA UKUNGA WA AJABU MPAKA NIKASHANGAA AKANIAMBIA MWANANGU UNA MIMBA UMEITOA WAPI? AKASEMA MIMBA MIMI SIJUI BAADA YA KUBANWA NA MAMA YAKE KUONGEA KWA UCHUNGU NDIO KUMUHADITHIA KILA KITU MAMA YAKE

MAMA YAKE NDIO KULIA SASA NITAMWAMBIA NINI BABA YAKO MIMI AKALIA SANA MAMA IKABIDI AMFWATE RAFIKI MPENZI WA YULE BABA NDIO KUMUELEZA UKWELI WOTE NA KUMUOMBA AKAONGEE NA YULE BABA NAYE AKAFANYA HIVYO

ANANIAMBIA ROSE BABA YANGU HAKUONGEA NA MIMI WALA KUPOKEA SALAMU YANGU NDANI YA MIEZI SITA BILA KUJUA MIMI SIKUJUA LOLOTE KUHUSU MIMBA, ANASEMA WAKAANZA KUMFWATILIA YULE KAKA WAKASIKIA ALISHAHAMA MAANA ALIJUA TU MSALA WAKE BASI WAKAANZA KULEA MIMBA MDADA WA WATU MIAKA 16

MPAKA WAKATI WA KUJIFUNGUA KWAKUA ALIKUA MDOGO NYONGA HAZIKUFUNGUKA IKABIDI AFANYIWE OPERATION ILI KUMTOA MTOTO NDIO KUJIFUNGUA SALAMA KURUDI NYUMBANI SASA

NDIO KULEA MTOTO WAKE, MTOTO ALIPOCHANGANYA AKARUDI SHULE AKAMALIZA NA KUPATA KAZI NA HADI KUJA KUMPATA MWANAUME MWENGINE NA KUMUOA

MAMA YAKE KILA LEO ANAJUTA KWANINI HAKUONGEA NA MWANAE KUHUSU UKWELI WA KUKUTANA NA MWANAUME...

BASI NA SISI TUKIWA KAMA WAKINA MAMA TUJIFUNZE ILI KUOKOA VIZAZI VYETU..

****END****


Reactions:

0 comments:

Post a Comment