Monday, June 2, 2014

MIYE NAWALETEA TU MJIFUNZE NAYO NIMEITOA HUKOOOO... KWA WANANDOA (NA MNAOELEKEA)

Naamini mliapa kuvumiliana katika SHIDA NA RAHA. Lakini sio katika TABIA MBAYA NA NZURI. Kwenye viapo vya ndoa, hamna sehemu ambayo mtu anaapa kuwa "nitakuvumiliya katika TABIA MBAYA NA NZURI." hUO NI UPUNGUFU WA FIKRA.
Wengi wetu leo wamegeuza kuwa tabia mbaya TENA SUGU za mwenzake kuwa ni sehemu ya MAMBO YA KUVUMILIYA bila kujua kuwa wanajenga msingi wa laana kwa kizazi chao na malezi mabaya, kwa kuvumiliana kwa mambo ya kijinga.
Mambo ya kuvumiliana katika shida na raha ni hali ya kiuchumi inapokuwa sio nzuri, magonjwa, na mambo yote ya raha. LAKINI SIO TABIA MBAYA ZA MKE/MUME, KUPIGANA KILA SIKU, MATUSI, WAKWE NAO WALETE YAO, MAWIFI WAZUE MABALAA, UASHERATI NA UZINZI nk yote hayo mtu anayavumiliya KISA NDOA.
HUO SIO UPENDO WA KWELI KATIKA NDOA HATA KIDOGO. Ndoa ni IBADA. Maisha ya ndoa ni kama mpo hekaluni mwa bwana mkiabudu. Na madhabahu yake ni KITANDA. Na ndio maana akasema "na malazi yawe safi."
1 WAKORINTHO 7:1-5
zingatia mstari wa 5 unasema.."Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda ili mpate FARAGHA KWA KUSALI; Mkajiliane shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.". Kwa hiyo MNAANZA KWA KUSALI KWA SABABU MPO MADHABAHUNI MWA NDOA, MPO IBADANI.
KUTENGANA
Kutengana kunakuja pale ambapo TABIA MBAYA NDANI YA NDOA ZIMEZIDI.
1 WAKORINTHO 7:10
"Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza, wala hapo si mimi ila Bwana, mke asimwache asiachane na mumewe. Lakini ikiwa wameachana naye, na akae asiolewe, au wapatane na mumewe tena asimwache mkewe"
Biblia imekuruhusu kwamba kumbe UNAWEZA KUTENGANA NA MWENZAKO atakapojirekebisha na ukiridhika kuwa amekuwa sawa MRUDIANE. KWANINI WEWE UENDELEE KUHARIBU IBADA TAKATIFU YA MUNGU?
Mungu amekataza KUACHANA akitumaini kuwa mtazifuata sheria na kanuni za maisha ya ndoa. MUME/MKE Muasherati, mgomvi, mtukanaji, mnyanyasaji, asiyetunza watu wa nyumbani mwake ANATENGWA NA KANISA. SASA KAMA KANISA LINAKUTENGA, UNA FAIDA GANI YA KUBAKI KWENYE NDOA KAMA SIO KUJITIA UNAJISI? Mume kupiga wake zenu, manyanyaso ya wakwe na mawifi na mashemeji alafu mwenzako hata hasemi kitu ilhali anaona wazi kuwa NDOA INAWEZA KUVUNJIKA, au hata kuhatarisha maisha ya mwenzako, UNAVUMILIA eti ni sehemu ya SHIDA ZA NDOA. NANI KASEMA?
FUNGUKENI VICHWA VYENU sio kuvumilia UPUMBAVU mkidhani ndio kuimarisha ndoa na upendo kumbe ni KUJIPANDIKIZIA LAANA NA CHUKI KWA VIZAZI VYENU.
Mjifunze NENO LA MUNGU sio kila kitu ni KUVUMILIA tu. MTENGANE KWA MUDA ILI KUMPA NAFASI YA KUJIREKEBISHA TABIA NA KUMALIZA KASORO ZILIZOPO.
NDOA NI IBADA TAKATIFU INATAKIWA IENDE KWA MISINGI YA UTAKATIFU. Lakini kwa sababu ya TAMAA ZA KIDUNIA tunajikuta tunamfanyia MUNGU UNAFIKI kwa kupitia NDOA. Mnasuluhisha matabia mabovu ya wanandoa lakini bado wako vilevile, kanisa linawatenga, lakini bado wako vilevile. Ukiwaambia wanasema NAMVUMILIA TU. MTENGANE KISHERIA KWA MUJIBU WA BIBLIA/NENO LA MUNGU.
ILA KWA KWA DHAMBI YA UZINZI NA UASHERATI HATA KAMA UNAMPENDA KUPITILIZA, HAPO NI KUVUNJA NDOA KWA TALAKA KAMA KWELI UNAISHI KWA KUMTEGEMEA MUNGU.

0 comments:

Post a Comment