Friday, May 30, 2014

WANAUME HII NI YENU...

Leo nije kwa wakina kaka. Kwakweli sikufahamu kuwa hadi miaka ya dot com bado watu wanakataa ujauzito na watoto, really???. Wakati unafanya tendo hilo na huyo dada hukujua matokeo yanaweza kuwa nini? Wako wapi vijana wanaojua thamani ya msichana na kumsubiri hadi siku ya harusi? Wako wapi vijana wanaosimamia na kuamini wanayoyasema? Vijana wa siku hizi wamejaa mashairi mazuri mno ya mapenzi, yani maneno yao yanawamaliza kabisa wadada hata wakilokole wanajikuta wametoa yote. Inapotokea mimba basi huruka mita mia, kama sio yeye kabisa, mashairi ya kubembeleza yanageuka mikuki ya kuchoma moyo!
Umeshamkosea Mungu, dada amepata mimba ni jukumu lako kuutambua ujauzito huo na kuulea pamoja na mtoto. Wengine wanawashauri wasichana watoe mimba na wasichana kwa kutokujua la kufanya wanakubali. Ni jambo la aibu sana kukataa mimba na mtoto wako, na akishafika miaka mitano unajitutumua mahakamani kumdai mtoto, mbaya sana.
Wewe kijana unayesoma hapa, Mungu anajua ni watoto wangapi umewakataa, Tubu sasa mbele za Mungu na haraka uende ukaombe radhi kwa mama watoto wako na ukubali majukumu yako.

Imeandikwa na: Women of Christ

0 comments:

Post a Comment