Monday, February 10, 2014

Looohhh yamemkuta shoga, vigezo na masharti kuzingatiwa...

kuna kaka mmoja shekh ameoa na anawatoto wawili, wanaishi vizuri tu na familia yake..

kama tunavyojuwa hizi dini zetu tunaruhusiwa kuoa mke wa pili ila kwa kukubaliana tu na mkeo wa kwanza na unaweza kufanya hivyo mpaka wake wanne

basi huyu kaka akawa amempenda mdada mmoja na kumuomba mkewe kama angeoa mke wa pili, kwa mapenzi ya mkewe wala hakuwa na gubu bali alimkubalia mumewe kuoa mke mwengine

bwana akapata mwanamke kweli kama tunavyojuwa mapenzi yanavyokuwaga motomoto mnapokutana, basi yakaenda hivyo miezi kama sita wakaanza process za ndoa

wanaume wakajipanga kwenda kutoa mahari kwa mwanamke, walipofika kwa mwanamke mbwembwe zao zote za kuoa naona zilifika mwisho maana walipewa masharti magumu sana

wakwe wakamwambia bwana harusi kwamba mtoto wao hali maharage, hali mlenda hali bamia..yeye anakula nyama,kuku,maini tu

dduuhhhh kusikia hivyo ndugu wa mwanaume wakaanza kunong'ona chini kwa chini lakini kwakuwa jamaa alikuwa ameshampenda binti akakubali na kutoa mahari ndoa ilikuwa imepangwa mwezi ujao Tanga

basi karibia na siku ya ndoa shoga akasafiri kwenda Tanga kusubiri kuolewa pamoja na ndugu zake na mashoga zake

kama mnavyojua shamrashamra za ndoa mara uchorwe piko ukae ndani usingwe na vitu vyoote kama hivyo basi haikuwa tofauti kwa huyu shoga

upande wa pili ndugu wa mume walikaa na kijana wao chini na kumshauri je siunajua ndoa za kiislamu ukioa lazima nyumba zote mbili uhudumie sawa kwa sawa

na kwakuwa huyu shekh yeye alikuwa na nyumba aliyopewa ya urithi walitaka wake zake wote wawili akae nao katika nyumba hiyo watenganishwe na vyumba tu

sasa ndugu zake wakamwambia unadhani itakuwa vizuri mke mdogo akipika kuku wakati mke mkubwa kabandika maharage na wote wapo nyumba moja huoni kama unajitia dhambi na kumnyanyasa mmoja

basi wakamsemaaaaa wee yule bwana mpaka akili ikamkaa sawa

siku ya ndoa ikafika mwanaume akasema haendi kuoa kwamba masharti yamemzidia kule shoga yupo mwenyewe anajipamba anajua anakuja kuolewa

subiri subiri na yeye waapi siku ikapita,wiki na hata mwezi ikabidi sasa arudi dar ili ajue kwanini ameachwa kwenye mataa

ndio bwana na ndugu zake kuwaambia wakwe wameshindwa na masharti, kwani yeye alitaka kuoa mke ambaye watakuwa wote kwenye maisha ya shida na raha lakini naona huyu hayupo tayari na sitaweza kummudu

wakaomba kurudishiwa mahari yao, na wakapewa baada ya siku mbili na ndio mapenzi yao yakaishia hapo

shoga yupo tu mtaani na mapiko yake anazunguka watu wanamnyali tu..wenyewe wanamuita mama kuku

******END*******




0 comments:

Post a Comment