Friday, September 13, 2013

Umesikiaa eeehhh

Niongee tena, kamwe asilani usifanye maamuzi ya kuoa au kuolewa kwa sababu ya kumuonyesha mtu kuwa wewe bado unalipa. Umekuwa na mtu kwa muda mrefu, ghafla anakuacha na kuoa au kuolewa na mwingine, tulia na usichukue maamuzi yoyote ya ghafla. Usifanye maamuzi ya kudumu kwa sababu ya emotions za muda mfupi, utajuta. Kuna watu walipoachwa wanaamua kuingia kwenye ndoa haraka ili kumuonyesha yule aliyemuacha kuwa bado wamo, hapo haumkomeshi mtu bali unajikomesha mwenyewe.
Wakati ukiwa kwenye maumivu ya kuachwa sio muda kabisa wa kuanza mahusiano mengine, subiri hadi moyo wako upone kabisa. Unaweza kujikuta unanzisha mahusiano na kuvunja kila siku, sababu ni kuwa moyo wako haujapona jeraha la kuvunjika kwa mahusiano. Ndoa sio kumuonyeshea fulani, ni maisha yako... Tumia busara.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment