Friday, September 13, 2013

Neno kuntu...

Unavunja mahusiano sababu kijana hana fedha, hana gari, hana nyumba nzuri.
Hivi siku hizi wasichana hawafanyi tena kazi za kuwapatia kipato? Iweje mali na gari viwe vigezo vya mchumba anayefaa? Yeye amepata wapi ambapo wewe umeshindwa kwenya kuvichukua? Yani imefika mahali vijana imebidi wadanganye na magari ya watu ili waweze kukubalika.

Kama unatafuta business partner, sponsor au investor kweli itabidi uangalie uwezo wake kifedha; ila kama unatafuta mume kuna mambo ya muhimu ya kuangalia na kamwe mali sio kigezo, mtu awe anafanya kazi halali ya kumpatia kipato na anamalengo na maisha yake tosha.
Fedha, mali na gari havifanyi ndoa idumu. Havileti furaha na pia si vitu vya kudumu.

Kutoka: Woman of Christ

Reactions:

0 comments:

Post a Comment