Monday, September 2, 2013

Kurasa za ndoa katika mzunguko...

Utafiti wa wanandoa kufanya tendo katika maisha yao ya ndoa kwanzia siku 1-mwaka mmoja wanandoa wanaenda mzunguko kwa wiki mara nne mpaka tano na haswa ambao hajaolewa akiwa na mimba, Miaka 2-3 hawa kwa wiki wanaenda mzunguko mara tatu, miaka 4-5 kwa wiki wanaenda mzunguko mara mbili na kwamiaka 5-na kuendelea kwa wiki wanaenda mzunguko mara moja na pia inawezakana wasizunguke kabisa hata wiki nzina wengine hata wiki mbili

KWANINI: Mwaka wa kwanza wa ndoa bado ndio mmetoka kwenye uchumba tena mwanzo mlikuwa mnaibia masaa ambayo mlikuwa mnakutana yalikuwa bado hayawatoshi kupeana raha kikamilifu kwahiyo mnapooana mnakuwa bado very active katika mzunguko na kuwa pamoja ukiangalia tena ndani ya nyumba mpo wawili tu bado hamjaanza kuumiza vichwa kwa majukumu makubwa kwahiyo mara nyingi mpo kwenye love mood kuwa pamoja, kubembelezana, kushikana, yani haubanduki kwa mwenzio.

Mwaka wa 2-3, hapa sasa ndio MUNGU amewabariki labda mwanamke umepata mimba, sasa kile kipindi chote cha mimba kama tunavyojuwa mwanamke unakuwa huna hamu ya mzunguko mara kwa mara na kwakuwa yule mwanaume na yeye ndio mtoto wake wa kwanza basi wote mpo kwenye furaha ya kuwa wazazi akili zenu na feelings zenu zinakuwa kwenye mimba na mtoto ajaye, kwahiyo mnajikuta mnahamishia mapenzi mengi pale mpaka mwili wako utakapojisikia hamu ya mzunguko ndio uombe upewe au pale mwanaume anapojisikia leo nahitaji kumpa mke wangu basi atakuandaa ili umpe.

Na kama ndani ya miaka hii mwanamke hana mimba mara nyingi wao kwa wao wanakuwa na mawazo kwanini hawapati mimba na wengine mpaka wanachoka kabisa mzunguko maana anajua akishazungushwa baada ya hapo wataanza kusikilizia kama mimba imeingia au la, kwahiyo idadu ya siku za  mzunguko zinaanza kupungua japo mkikutana mnahakikisha iwe hodari yenye kuchangamka..

Miaka 4-5 hapa sasa ndio miaka ile wenye ndoa ndio wameshazoeana kupita kiasi hekaheka za ndoa zimeshawachanganya mpaka sasa wewe ukipewa sawa usipopewa sawa, miaka hii ndio wanaume wanapocharuka kwa kuwa na wanawake nje, wanaume ni watu wa kuchoka na kukinai tofauti na sisi kwakuwa sisi wanawake tunapenda kwa MOYO yani hata miaka mingapi bado utampenda mumeo kama mmelandana lakini wanaume wanapenda kidogo kwa moyo ila zaidi kwa matendo kwahiyo anapokuwa ameshakuwa na wewe miaka mpaka minne anakuwa anakinai anatafuta kitu fresh kutoka nje na ukichunguza hiki kitu hata siku moja mwanaume hawezi kumuacha mke wake na kwenda kutongoza tena mke wa mtu huwa wanaenda na young blood, msichana wa chuo, ama ambao hawajaolewa kwahiyo huko anachangamshwa akirudi nyumbani kwakuwa ameshamzoea mkewe anampa tu mara moja au mbili tena ni bao moja tu kwa wiki

Miaka 5 na kuendelea hapa ndio inaitwa ndoa iliokomaa sisi tunasema kama ndoa yako haijavunjika ndani ya miaka mitano basi itadumu sana labda litokee jambo mbele ambalo haliwezi zuilika, hapa sasa mnakuwa mnapendana ki mwili ndoa yenu inakuwa na mambo mengi ambayo nyie wawili mnayapenda na kutaka kuyaendeleza zaidi kuliko mzunguko hapa sasa mzunguko ni asilimia ndogo sana inayoongoza ndoa ila kubwa ni upendo wa ukweli hapa ndio pale mwanamke mumeo anarudi anakubusu na kukumbatia anakuonyesha mapenzi tele wewe na watoto na anaweza asikuzungushe wiki nzima na wala usione kama ni mbaya...

Unapotaka kuwa mke wa fulani au unapokuwa kwenye ndoa tambua upo kwenye kurasa gani na vipi ukae na mumeo sio kila mara mwanaume anapokuja nyumbani na hajakuzungusha basi amezungusha nje hapana huyo atakuwa mwanaume wa aina gani kila siku ya MUNGU anazungusha tuuuuuuuuu

Tujitahidi wapendwa kubebea misalaba ya ndoa zetu na tujue kuishi na wame zetu vyema na tutumikie ndoa zetu...

Reactions:

0 comments:

Post a Comment