Thursday, September 26, 2013

KAMA SIO LAKO HILO BASI LA JIRANI YAKO


Umetokea kumpenda mkaka, unatamani akuambie anakupenda lakini yeye anakuchukulia kama rafiki wa kawaida. Kwasababu ya urafiki wenu anakueleza kuwa kuna msichana anampenda, au tayari yupo naye na wewe sababu ulitaka awe wako unaanza kumsema vibaya huyo msichana ili huyo kaka amchukie. 

Tabia hiyo ni mbaya sana sana. Hata kama unayoyasema ni kweli sio yako ya kuyasema, muache ayaone mwenyewe. Unajuaje kama ndiyo aliyompendea? Kwanini kusema past ya mtu bila ruhusa yake? Itakusaidia nini? Kama kweli huyo dada hafai muombe Mungu amfunulie huyo kaka na sio wewe sababu ya hisia zako umharibie msichana mwenzio. Unajuaje kama hajabadilika? 

Na wengine husema ya uongo kabisa ili tu msichana wa watu aonekane mbaya. Kama unatabia hiyo nakusihi kwa jina la Yesu uache kabisa maana haipendezi na usifikiri kwa kufanya hiyo ndipo huyo kaka atakuwa na wewe. Anaweza kumuacha huyo msichana na kumuoa mwinginee na sio wewe.


Imeandikwa na: Woman Of Christ

Reactions:

0 comments:

Post a Comment