Tuesday, September 10, 2013

Chezea SOMO/mc Sophy weye...ARUSHA tunakuja....

Mashoga zangu wa Arusha mpo hehe heiya chezea siye weye kushoto somo Sophy a.k.a chumvi chumvi  kulia miye mwenyewe, chezea watoto wa Temeke na Mabibo uswahilini kwetu siye na mambo yetu tunayajua siye...halooooooo

Tutakuwepo Arusha kuja kuwafunda wanawake wa Arusha aliyesema kilimanjaro wagumu kama gogo nani bibi wee ilikuwa zamani siku hizi wanawake wote walaini watoto tentemente..bibi wee kama wewe upo Arusha, Moshi na sehemu zote za jirani karibuni kufundwa bibi chumbani shoga yangu tupo huko siku tano kwanzia 4,5,6,7,8 mwezi wa kumi kuja tu kuwanoa... 

Shoga sasa chagua tarehe yako wewe na mashoga zako mje kufundwa hii ni ya kiutu uzima ndio maana hatufanyii nje ukiingia ndani unapewa khanga yako unakaa style ya kufundwa maneno utapewa na goma utachezeshwa kama hutaki utaangalia tu sitaki kuongea mengi humu utaja jionea mwenyewe siku zenu mlizochagua..

Shoga chagua siku yako na kama mpo wengi niambie mpo wa ngapi mtapangiwa siku yenu peke yenu hamtachanganywa na wengine ila kama upo peke yako itabidi uingie na wengine ambao wa chache, ukishajuwa mnataka kuja lini nipigie 0717 019320 kiingilio ni 30000 kwa mtu mmoja uweke siku yako Mapemaa..

Mliniomba nirudi tena nilivyokuja mwezi wa pili na nikawaahidi nitarudi ndio hivyo naja...hehe heiya mwanamke kujishebedua bwana sio unajishaua ukilala unalala kama mti, mwanamke ukilala na mpenzi wako usiku taa imezimwa tukapapasa miili hujui mwanamke yupi mwanaume yupi...mtoto wa kike hujafundwa weye...

Hahahahaha halooooo tukutane siku hizo na kama unaaibu naomba usije kutuharibia siku maana wapo ambao hawajui na wanataka kufundishwa, hakuna kuchekana ukicheka tunakutoa nje na huingii tena ndio maana tunafanya chumbani sasa hivi hata asiyejua ajifunze...

Siku ni chache wahi yako mapema...


Reactions:

0 comments:

Post a Comment