Monday, July 22, 2013

Uswahilini kwetu..

Jamani ngoja niwape kisa cha uswahilini kwetu, kuna dada mmoja ameolewa na anawatoto wawili, kutokana na matatizo ambayo amepitia kwa muda mrefu na mumewe ikafika kipindi akaacha kabisa kumuamini mumewe, japo kuwa mumewe anacheo tu kikubwa serikalini na anahela maana wananyumba tatu na biashara nyengine nyingi tu.

Sasa huyu mumewe jamani anavituko sana kwanza labda kwa vile ni kabila lao lilivyo ila pia sidhani labda wanasingizia tu kabila la wakuria ya kwamba kwanza yeye mke wake si kitu mbele yake zaidi ya kumzalia watoto na kuhakikisha nyumba ipo kwenye hali nzuri.

Huyu mama anasema amekuwa akivumilia hayo matatizo ya kudharauliwa na mumewe kwa muda mrefu saa, tena unaambiwa hata kwenye vikao vya familia wanawake kwao hawaruhusiwi kuongea wala kuchangia lolote wao ni kukaa tu tena ukiheshimiwa na kusikiliza.

Huyu mama kuona hivyo na kwakuwa kama nilivyowaambia ni mama wa nyumbani akaamua kujipanga, hizo hela alizokuwa anaachiwa na nyengine anajuwa alipokuwa anazipata akaanza kutafuta biashara zake za pembeni ambazo mumewe hazijui, akafungua salon, akanunua bodaboda tatu, na sasa amefungua mgahawa mzuri tu..KUMBUKA bila mumewe kujuwa.

Sasa hapa katikati wamegombana na mumewe na akaamua kuondoka na watoto kwenda kukaa kwa kaka yake ambaye ameoa na anawatoto wawili na kaka yake huyo anaishi kwenye chumba na sebule, ameacha maisha mazuri tu kwa mumewe kisa huyu baba anamdharau na pia huwa anampiga sana mpaka kulazwa.

Tukimuuliza kwanini hataki kwenda kupanga anasema anaogopa huyo baba akija kupajuwa alipopanga basi atampiga sana, sasa ameamua tu kuishi hapo kwa kaka yake, mke wa kaka yake ni rafiki yangu sana mtaani sasa akaja ndugu ya huyu dada kumueleza juzi kwamba kule nyumbani kwake mdogo wake wa kike anayemfwata amehamia anaishi na shemeji ambaye ndio mume wa huyo dada!!!!!!!!!!

Hahahaha sicheki kwa kuwa ni mazuri ila nilishangaa jinsi huyu mdogo mtu alivyokuwa na guts mbaya yani dada yako kaacha nyumba yake kwa sababu ya matatizo halafu shemeji yako anakuita na unahamia huko eti kisa ukalee watoto wa nje wa huyo baba aliowapata kabla hajamuoa dada yako!!!!!! mimi hainiingii akilini sijui wewe msomaji wangu.

Sasa mimi nikamwambia kitakachofwata mdogo wako atakuwa mke mwenzako na lazima shemeji atakuwa anakula japo kwa kuiba..akaniambia aibe mpaka amzalie pale sirudi na yeye si mwanamke muache akajionee...ila siruidi msinipe kabisa habari za kwenda kumvumilia mwanaume asiyeona umuhimu wangu

Kwahiyo shoga bado tunaye uswahilini kwetu, ila siye wanawake hapana aisee yani ukaishi nyumbani kwa dada yako wakati yeye hayupo anamatatizo na mumewe kisa ukalee watoto wa nje wa shemeji yako ambaye hajazaa na dada yako...yani huyu dada anahitaji kuchapwa!!!!!!mfyuuuuuuuuuuu (msonyo)