Tuesday, July 23, 2013

Migogoro...

Migogoro ya familia siku hizi imekuwa ni jambo la kawaida maana mara kwa mara tumekuwa tukisikia na migogoro ya aina hii ni ipi naongelea ya ndoa pindi mume anapokuwa amefariki..

Kwanza kabisa wanaume wengi waliumbwa na ubinafsi na ndio maana mume anapokuwa amekufa mke wake ananyanyaswa tena hii ni mbaya zaidi kwa mwanamke ambaye hana kazi yeye ni mama tu wanyumbani, utakuta mwanaume ananyumba na mali nyengine lakini yeye hata siku moja hamshirikishi mkewe kwenye mambo yake yeye anachofanya kila kitu anaeleza ndugu zake mkewe hamuelezi jambo lolote yeye anaona tu vitu vinafanyika ama biashara zainaongezeka tu.

Kwakweli hii ni mbaya hata kama mkeo hana uwezo wa kufanya kazi na kuingiza kipato ule ndio ubavu wako MUNGU amekupa, angeweza pia kukufanya kamwe katika maisha yako usioe uwepo tu mtaani, alikuwa na uwezo wa kuwachukua ndugu zako wote na akakuacha na mkeo tu ila amekupa mke ili awe msaidizi kwako sio tu kukuzalia watoto na kukufulia nguo na kuhakikisha umekula bali kuwa msaidizi hata katika kukujenga kimaisha na kiroho pia.

Mimi huwa nasikitika sana kuona mwanake amefiwa na mumewe halafu ndugu wa mumewe wanamnyang'anya mali zote huyo mama na kumfukuza pamoja na watoto wake!!!!!! kweli jamani yani ushemeji mliokuwa mnamuheshimu wakati ndugu yenu yupo leo mmemfanya kama mgeni kama hamjawahi kumuona hapana aisee...sasa na ile damu ya ndugu yenu mnaiacha tu ipotee izagae bila msaada huku nyie na watoto wenu mkifurahia mali alizochuma kaka yenu na mkewe tena utakuta wakati anachuma mkewe alikuwa hamuachii hata hela ya kula wanalala njaa ili mradi wanaamini ipo siku watapata sasa wamepata ndugu yenu hayupo mnamnyang'anya mali zake!!!!!! hapana aisee

Ni bora wewe kama mume ukawa na msimamo wako kwamba jamani mimi nimeoa leo sipo mali zangu na waachia watoto wangu kwa usimamizi wa mke wangu mpaka watakapokua na umeiandika kabisa chini na muhuri wa mwanasheria juu ili yule mama ambaye hajaui kujitetea siku wakimfukuza anauwezo wa kwenda kushtaki mbele ya sheria na akaonyesha udhibitisho na kutetewa.

Ndio maana siku hizi wanawake wameamka hata kama ameolewa atachacharika kutafuta vyake ili hata kama kesho jamaa haupo yeye maisha yanasonga, na wanawake wa mjini wanajuwa kujitetea jamani eti umdhulumu mali alizochuma na mumewe hakunaga labda umtoe roho kwanza.

Kwahiyo wanaume jamani wakati huu ukiwa bado hai jipange vizuri na mkeo na ndugu zako kwani hakuna anayejuwa lini ataiaga hii dunia, na pia kwa wanawake ambao mna mali pia nanyi mjipange sio unakufa ndugu zako wanakuja kudai hiki kiwanja alipewa dada yangu kwenye sendoff tunakitaka INAHUSU...

Reactions: