Sunday, July 28, 2013

Kumbe......

 Hapa ndipo ninaposhindwa kuwaelewa wanaume, yani wakifanya wao ni sawa akifanya mwanamke kakosea...

Jamani sitaki kujitetea pamoja na wanawake wengine na wala usidhani ni mashindano na wala sipo huko kabisa ila tu nataka kuongelea hili swala leo, kwanza kabisa wewe mwanaume hakuna kitu kibaya kama wewe unapiga mechi za nje halafu mkeo akagundua..ngoja niwaeleze kitu sisi wanawake ni watu wa kuvumilia sana tena sana utafanya kila kitu kibaya kwa mwanamke lakini atakuvumilia kwakuwa MUNGU alitumuumba sisi wanawake kustahimili yote ya dunia lakini tunakuwaga na mwisho wetu siku mke wako akisema basi ni basi na huwezi kumrudisha nyuma na hata kama akirudi nyuma itakuwa sio kama mwanzo.

Wewe mwanaume unapiga mechi za nje, wanaume wenyewe siku hizi nguvu za kiume hamna unajititumua nje unapia bao tatu halafu unarudi kwa mkeo unalala kama kitanda cha mama yako kile na uliye lala naye ni dada yako unategemea nini??? na mkeo pia ni binadamu anamahitaji yake ya kimwili tena siye wanawake usipopindwa tu ndani ya mwezi au miwili unaumwa sana tumbo na kuchakaa sura kwa chunusi..inahusu nini sasa kuchakazwa sura mjini hapa..ebooo

Hapo ndio mkeo na yeye anachoka sasa maana unavumilia mpaka mwisho unaona hapana kuna rafiki yangu mmoja aliniambia "shoga yangu dawa ya mwanaume ni mwanaume mwenzake"...nilimshangaa akaniambia mpaka siku ya kikukuta ndio utajuwa dawa hii kama ni super....

Ndoa za siku hizi zimekuwa ngumu wengi wanaamini hivyo lakini ugumu na wepesi wa ndoa upo mikononi mwenu unaweza ukapiga mechi za nje na mkeo ukampaa vilevile atagunduaje lakini jitie wewe mjuaji uisome junejuly..na wanawake wakitoka nje ya ndoa ni noma maana kwanza sisi wanawake ni wepesi sana kupenda na mwanamke akimpenda hawara atashindwa kabisa kumuhudumia mumewe ndani sio hawezi hana hamu yani yeye kulala na wewe kama kaka yake hajionei tabu, na pili hata akikupa atakupa huku kafumba macho akimuwaza hawara yake ili apate raha, maana kwako ni chuki tu atakuwa nayo na ili usijuwe atakupa huku akigunia uroda wa mwezio anaoupata nje..ukijitia wewe mwizi ujuwe mwenzio ni jambazi kakuzidi maarifa

Kwahiyo sasa inahusu nini wewe mwanaume ukajipe mapresha na kuuwa au kuumiza watoto wa mwanaume mwenzio kisa kakusaidia kukutunzia mkeo kazi ambayo wewe mwenye mke umeshindwa kuifanya...tena wewe ukihisi mkeo anamtu nje na sababu ni wewe unatakiwa tu kuwa mdogo sio kuleta ubabe, tena umuombe mkeo msamaha kwa kushindwa kuwa mume bora mpaka akatafuta bora mwanaume...

Mwanaume tafakari hilo...

Reactions: