Wednesday, July 31, 2013

GODORO....

Leo nataka kuongea na wanawake haswa wale ambao hawajaolewa bado na sio mbaya kwa wale walioolewa labda na wewe ulikuwa hujui likakusaidia.

Unapokuwa unaolewa mama yako au ndugu zako wanakupa godoro, hivi wewe unajuwa lile godoro ni la nini ndio najuwa unajuwa ni la kulalia lakini kulalia vipi unafahamu au ndio ukifika kwa mumeo tena mnaliweka kwenye chumba cha wageni ili wakija walalie au tena ndio mnaweka chumbani kwa dada alalie sindio????

Godoro mtoto wa kike unapopewa na mama yako unatakiwa ulalie na mumeo yani lile lililopo chumbani kwa mumeo ukalitoe upeleke chumba kingine na hilo ulilopewa ndio uweke chumbani kwako mlalie, mama anavyokupa godoro ni sehemu kubwa katika maisha yako ya ndoa.

Wewe sio mwanamke wa kwanza mumeo amkeuwa naye ndio akakuoa, kuna wengine kibao walikuwepo mbele yako na inawezekana hata watano tu wameshalalia hilohilo godoro na kufanya majamboz yao humo, wanawake wengine ni wazuri katika kumloga mwanaume na sehemu kubwa huwa ni godoro wanachomeka vitu vyao vingi chini ya godoro ili kumkamata mwanaume, sasa wewe shoga hujui unaling'ang'ania godoro la mumeo..inahusu

Kama hukulijuwa hilo ndio ulifahamu sasa.. kama hukupewa godoro wakati unaolewa basi ununue godoro jipya ndio mlalie.