Wednesday, June 5, 2013

Yako hii Mke..

Hivi sisi wake ambao tumeolwa na tunafanya kazi nyumbani tunaacha nyumba zetu na watoto wetu tena wadogo wakiwa na msichana wa kazi na tukirudi tunawakuta salama je wewe kama mama unakaaje na msichana wako wa kazi unampenda ama unamchukulia poapoa sikia kisa hiki...

Kuna dada mmoja maeolewa na anawatoto wawili mmoja miaka miwili na mwengine mwaka huyu dada akaagiza msichana wa kazi na akaletewa mtoto mdogo tu mwenye miaka 16 ambaye alikuwa yatima akilelewa na bibi yake.

basi unajua watoto wa umri ule ni bado wadogo wasumbufu na wamefuatana kama mapacha sasa dada alikuwa akiona wanalia anaacha kazi anavibembeleza kwanza,anachofanya anawasha tv anawaonyeshea ili watulie maana kuwabeba wote hawezi.

 kumbe shoga akifika nyumbani akikuta labda kuna kazi hataki kusikia la mwazini wala kardinary pengo matusi,masimango mtindo mmoja mtoto anavumilia akikumbuka kamwacha bibi wazazi hana ila uvumilivu una mwisho.

  basi siku hiyo katoka job kufika nyumbani dada hajamaliza kupika kisa watoto wanalia saa moja always watoto huwa wanasumbua usingizi,dada alichofanya kamtwanga vibao vya mwiko vzr tu msichana kalia kanyamaza kumbe usiku akayapanga yake.

asubuhi ilikuwa jumapili best haendi job wamelala kama kawaida dada kaamka kumbe ana hasira kalala nazo,kapika chai akaweka sumu akafunga kwa thermos chakula cha mtoto akakiweka sumu pia.

  MUNGU saidia mama mtu anaamka anaenda jikoni anaona chakula cha mtoto kina weusi kumwuliza dada akajibu karot zilikuwa nyeusi zimekaa mama mtu akakimwaga,basi akatengeneza kingine wale waliolala kuamka kuoga wako sitting roo wanakunywa chai baba na yule wa miwili balaa ikaanza tapika tapika.

 ikabidi tafrani wawahishwe agakhan ikagundulika sumu wakalazwa kama siku tatu msichana akajiondokea fasta iringa wakatoka hospital, basi bidada wambea wakamtonya mume kuhusu ukweli wa mkewe kumnyanyasa mfanyakazi mume alichofanya alimwachisha kazi marufuku house girl alee mwenyewe wanae.

Je wewe mke unamtunza vipi msichana wako wa kazi haya yote na mengine mengi yanayohusu ndoa zetu tutayaongelea na kuyatafakari pamoja 7/7/2013 palepale Majestic Hall Sinza kwa Remmy saa 5:00 asubuhi mpaka 12:00 Jioni usikose kwa kiingilio 30,000/- tu lipia kabla upewe ticket yako mapema bila ticket hakuna kuingia.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment