Wednesday, June 26, 2013

Neno...


Linda sana moyo wako kuliko vyote ulindavyo maana ndiko zitokazo chemichemi za uzima. Hayo si maneno yangu bali ni maneno kutoka kitabu cha mithali. Moyoni ndipo uzima wa mtu unapoanzia na moyo huharibiwa na vile tunavyoulisha kwa maneno, mawazo, na matendo. Na vitu unavyovipa muda mrefu ndivyo unavyoviwaza na ndivyo vinajenga au kubomoa moyo wako.

Unachat nini kwenye simu usiku na mchana? Page gani ume like na kuziangalia facebook? Blog zipi unazifuatilia kila siku? Huwezi kila siku kufuatilia page zenye picha na habari chafu na kuangalia blog mbaya na kutegemea moyo wako kutoa uzima. Siku nzima unachat about sex, je unategemea nini? 

Wengine wameokoka na wanachat kuhusu sex usiku na mchana. Biblia inasema usiyachochee mapenzi, hivyo ni makosa mbele za Mungu na ni kuwaka tamaa. Linda moyo wako, wewe ndiwe unauwezo wa kuulinda, acha kuwaza na kutamani juu ya sex wakati hujaoa au kuolewa "Natamani ungekuwa umelala hapa pembeni yangu","siku kama ya leo weekend hatutoki ndani ni bedroom tu","naenda bafuni I wish ungekuwepo tuende wote","how will you do me?"... Message hizi na nyingine mbaya zaidi unakuta watu wanaosema wameokoka wanachat na wapenzi wao maana huwezi kuita wachumba. Acha kabisa kuwaka tamaa ni dhambi mbele za Mungu.

Biblia inasema msiifuatishe namna ya dunia hii, na pia ikimbie zinaa. Mtu unayechat naye hivyo ni rahisi sana kuanguka naye dhambini maana kihisia mlishazini muda mrefu. Chunga sana mawazo ya moyo wako na maneno ya kinywa chako na jitahidi vipate kibali mbele za Mungu.


Source: woman of Christ

Reactions: