Tuesday, June 4, 2013

Majanga...

Kwa wale warembo wenzangu mnaokwenda Mwenge kusuka nywele zenu kama mie, jamani hii ni habari ya kuaminika kwamba, wale wadada wanaita " Dada karibu usuke" , kumbe sio wote ni wanadamu. Nasema hivi, wale wasusi wa yebo yebo kule mwenye, jamani, mengine kumbe ni MAJINI. Kuna mdada kasuka nywele zake, kapendeza, kichwa kimeumaaaaaaaaaaaaaa mpaka akazimia wakadhani pengine msusi amekaza mishipa ya fahamu imekandamizwa, kumbe, ALISUKWA NA JINI. Nasema hivi, wandugu wakamkimbiza hospitali, hawaoni kitu, kapelekwa kwenye maombi, PEPO likasema wazi kabisa kwamba " sikaja kwangu kusuka alitegemea nini"? Wapenzi, hii sio hadithi ya kubuni ni uhalisia, kwa hiyo mnapoenda kusuka, hebu muwe mnasali mkiwa makwenu, ombea msusi yule atakayekusuka na na rasta utakazosukia pia ziombee! Asomaye na afahamu!

Stella

Reactions:

0 comments:

Post a Comment