Monday, June 17, 2013

KINACHOPELEKEA WIVU KWA MPENZI/ MUME NI KITU GANI?JE WIVU NI MZURI?NIFANYEJE NINAPOKUWA NA WIVU?

HILI NI SWALI AMBALO KILA MMOJA ANAJIULIZA, NA WENGINE WAMEJIKUTA WAKIWA KWENYE HALI YA WIVU KWA KIPINDI KIREFU SANA, NA WENGINE WANAFIKIRI LABDA WIVU UNAWEZA KUEPUKIKWA, KAMA WENGINE WANAVYOFIKIRI KWAMBA VIVU HAUEPUKIKI.. HAYA NI BAADHI YA MAMMBO AMBAYO KILA MMOJA AMAKUWA AKIJULIZA SANA ANAPOKUWA KWENYE MAHUSIANO NA NI HALI AMBAZO ZINAMTOKEA.

WIVU UNAWEZA KUWA MZURI NA UNAWEZA KUWA MBAYA, WIVU UNAWEZA KUTENGENEZA NA UNAWEZA KUHARIBU NI LAZIMA HIVI VITU VIWILI VICHUKUE NAFASI UNAPOKUWA NA WIVU NA UNAPOKUWA UNAENDESHA PENZI/ NDOA.

LAKINI PAMOJA NA HALI HIZO ZOTE MBILI KUWEPO, ZA KUHARIBU NA KUTENGENEZA, JE LIPI LINALOONGOZA? UWE WIVU WA KUHRAIBU AMA WA KUTENGENEZA? TUNAPOSEMA WIVU WA KUTENEZA NA WIVU WA KUHARIBU ZOTE NI WIVU, ILA MATUMIZI YAKE AMA NAMNA YA KUENDESHA WIVU HUO NDIVYO VINAVYOFANYA SASA UHARIBU AMA UTENGENEZE.

WOTE TUNAJUA KWAMBA PAMOJA NA KWAMBA WIVU HUHARIBU AMA HUTENGENEZA LAKINI WIVU KAMA WIVU UMEBEBA: 1. Choyo, 2. Kujipendelea, 3. Kuhitaji, 4. Kutamani, 5. Hasira 6.Kuhudumia 7.Kupenda 9. Kubana , 10, Kutawala nk.. Hivi ni baadhi tu ya Vionjo vilivyopo katika WIVU.

VIONJO HIVYO KUMI NA VINGINE VINGI KULINGANA NA MTU WENYE WIVU AMA MHUSIKA WIVU NDIYE SASA HUWEZA KUFANYA WIVU UKAZAA KUHARIBU AMA KUTENGENEZA,,, KWA NINI TUNASEMA KUHARIBU AMA KUTENGENEZA? Assume mwenye wivu akawa na Hasira, Kujipendelea, Kubana, Kutawala na choyo? nini kitazalika hapo? Bila shaka ni Zaidi ya Kuharibu,, lakini turudi upande wa pili,, mwenye wivu huyo huyo, akawa na Kupenda, Kutamani, Kuhitaji, Huoni kama atakuwa ANATENGENEZA?

HIVYO BASI, TUNAPOFIKIA KWENYE KUULIZA JE WIVU NI JAMBO ZURI? Jibu lake lazima liwe hivi.... Bila wivu hakuna mapenzi,, na ambaye hana wivu na mpenzi wake basi hana mapenzi ya dhati kabisa,, hili ndilo jibu la swali hili... Wivu ni mzuri na katika mapenzi wivu wahitajika sana,, Hivyo mtu usiogope wala kujizuia kuwa na wivu hata kidogo, wala hakuna baya ufanyalo ila ni upenzi unaokusukuma.. Lakini tunapokuja kwenye swali la pili NIFANYEJE NINAPOKUWA NA WIVU? Kuna njia nyingi za kufanya unapokuwa na wivu, ili sasa wivu wako usiwe ni wa kuharibu ila wa kutengeneza, na wengi hapa ndipo wanapokosea... Ufanye nini? Unapokuwa na Wivu unachotakiw kukifanya ni kuwa na VIONYO Vifuatavyo kwenye wivu wako : 1. Mtamani sana mpenzi, Mhitaji sana mpenzi, mhudumie sana mpenzio na mpende sana,, kwani ukiweza kuwa na wivu wenye vionjo hivi humfanya apende kuwa karibu na wewe, hali ambayo itakufanya uridhike.

Nini kinachowashinda wadada wengi wanapokuwa na wivu? wanakuwa wachoyo, hasira, kutokujali nk.. na wanapokuwa na vionjjo hivi mara nyingi huharibu na huwa kero, lakini wanapojikuta wanakuwa na wivu uliobeba vionjo tajwa hapo kwenye comment ya juu ya hii, unajikuta wivu wako mpenzio anauthamini na unaridhika na kuepusha shari migogoro na magomvi. Hivyo ni lazima muwe makini katika kutumia wivu wenu.

KINACHOPELEKEA WIVU KWA MPENZI / MUMEO NI NINI? Kinachopelekea wivu kwa mpenzio, Mumeo ni kwanza kabisa ile hali ya kujihesabu MMILIKI HALALI... Ndio maana tunashauri ni bora kuwa na wivu kwa Mume ili hali kuna vigezo vinakulinda na kuna mambo ambayo yatakupa kufanya wivu wako kuulimiti ama kuuendesha utakavyo usilete madhara kuliko kuwa na wivu kwa mpenzi.. Hivyo Basi, hakikisha kwamba UNAPOKUWA NA WIVU ILI USIUMIE NI LAZIMA UWE MMILIKI HALALI.. Kwani unapokuwa sasa sio mmiliki halali unajikuta mara nyingi unaumia na kusononeka kwa wivu.. na ndio maana wakati sisi tunafundwa katika masuala ya kuingia kwenye mapenzi, Tulipewa ILANI ya kutomuonea wivu kijana ambaye huna uhakika kwamba atakuwa mpenzi wako wa kudumu... na ndio maana unapokuwa na wivu kwa kijana fulani ULIYEJIMILIKISHA WEWE BILA KUWA MMILIKI HALALI, unaendelea kuwa na wivu naye hata mkiachana (wale ambao mmekuwa na wapenzi mliojimilikisha na ikatokea mkaachana mtakuwa mashahidi kwamba hadi sasa mnawakumbuka na kuwaonea wivu.. hahahahahhaa.... sorry though)

UNAPOKUWA NA WIVU NA MUMEO NI RAHISI KWANI KUNA WAKATI ATAKUWA NA WEWE KARIBU KWA NJIA YA ULAZIMA,,, HIVYO BASI ANAPOKUWA NA WEWE NDIPO PALE SSA TUNASEMA WIVU WAKO UWE WA KUHITAJI, KUTAMANI NA KUHUDUMIA,, UNAPOMTAMANI, UTAMHITAJI UNAPOMPATA UTAMPA HUDUMA, NA KWA VILE SASA UTAFANYA KWA KUMAANISHA, KUNA UWEZEKANO MMKUBWA MHUSIKA HUYO ANAYEONEWA WIVU AKAJIKUTA ANAPENDA KUKAA KARIBU NA WEWE HAIJALISHI UNA WIVU KIASI GAANI LAKINI TU KWA SABABU UMEBEBA VIONJO TAMANISHI...


Reactions:

0 comments:

Post a Comment