Friday, June 7, 2013

Hatareeee ni wakati wetu tena....

 Hehe heiya wako wapi wanawake walioolewa haya sasa huu ni wakati wetu bibi siye wenye ubavu wetu ndani hatukopeshwi wala hatuazimi wa mtu bali wa kwetu wenyewe mpaka mbingu zinatambua.

Ni siku yetu wanawake tulioolewa tutakuwa pamoja kwenye mafundo, tena sio mafundo tu bali mafundo ya kiutu uzima tukichambua kurasa moja moja ya ndoa na kurasa kuu ikiwa ya chumbani na jinsi ya kumuhudumia mume..tunajuwa kitchen party tuliambiwa juu juu lakini hapa tutaonyesha mpaka mifano na kufundishwa kwa undani zaidi..haloooo

Somo yetu siku hiyo atakuwa bi Rehema mama wa lindi mwanamke aliyefundwa akafundika wiki mbili siku kumi na nne ndani akionyesha kumlea mume huyo ndio somo yangu miye kwake mwanamke aliyeolewa akifundwa kwake hakuna kuachika bibi wala mume kukusumbua anakupa mbinu zote za kuibeba ndoa yako na kumlea mumeo..bibi mwanamke uliumbwa msaidizi wa mumeo unajuwa kumsaidia ama unayumbayumba tu na yadunia hehe heiya...shoga usikose

Kwa wale wavivu wa mambo ya chumbani huku kutakuwa na dawa yenu mtafundwa, mtaonyesha na kupewa zana za kuingilia chumbani bibi nisije kukumalizi uhondo nunua ticket yako sasa ticket zishaanza kutolewa...hahahahahaha kama unadhani ulifanyiwa kitchen party njoo uone hii halafu ujipime...

Itafanyika 7/7/2013 kwanzia saa 5:00 asubuhi - 12:00 Jioni wapi ni palepale  Majestic Hall Sinza kwa Remmy ikisimamiwa  na captain wenu mwenyewe mtoto wa Kichagga Rosemary Mizizi hehe heiya kwa mnaonijuwa mnajuwa mambo yangu shoga uchagga mwisho chalinze Dar es Salaam wote wazaramu bibi...

OOhh miye siwezi kukata nyonga bibi nyonga hamna ya kichina lazima ujitegemee hayo na mengine mengi kuhusu ndoa yako utafunzwa  haloooooo chezea wanawake wewe... 30,000/=(utakula na kunywa)  lipia ticket yako sasa nipigie 0717 019320 kwa zaidi ya watu watatu nitakuletea ama tutakutana sehemu ya karibu nikupe ticket zako, hakuna sare vaa tu kwa ukaaji wa starehe maana tutakaa chini kwenye mikeka hiyo ndio heshima ya wanawake wanaofundwa.

Reactions:

1 comments:

  1. Burudani kutoka kwa kibao kata kitakuwepo, shoga una nyonga tutakuja kuiona, wale wanawake wenye viuno vyao pia watakuwepo na wao walioolewa tu ndio watatuonyesha show...hahaha sio ya kukosa hii

    ReplyDelete