Tuesday, June 11, 2013

Biblia na Mapenzi...

Wimbo bora. 2:7 
"Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe."

Wimbo bora 8:4 
"Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwani kuyachochea mapenzi, au kuyaamsha, Hata yatakapoona vema?"

Kitabu cha wimbo uliobora kimejaa mashairi ya kimapenzi kwa watu waliokwenye ndoa na wale ambao wanaelekea honeymoon. Katikati ya mashairi haya mtunzi amewaasa binti za yerusalem yaani binti wanaomjua Mungu kutochochea mapenzi wala kuyaamsha hata yatakapoona vyema. Ni wakati gani yanaona vyema? Wakati ukiwa kwenye ndoa maana ndio wakati ambapo Mungu ameruhusu mwanamke na mwanaume kuhusiana kimapenzi.
Kwanini amewasihi binti peke yao? Sababu ni ukweli usiopingika kuwa bint unanafasi kubwa sana katika kuchochea mapenzi. Ukiwa na mchumba unapaswa kuulinda utakatifu na kutokuongea, kuchat mambo yanayochochea mapenzi. Wanaume ni rahisi sana kufikiria kuhusu jambo hilo na kukutext, wewe kama bint onyesha msimamo kwa kutoendeleza mazungumzo ya aina hiyo maana ni rahisi kuwaingiza mtegoni.
Nakusihi ee bint uliye mpokea Yesu, usiyachochee mapenzi hadi yatakapoona vyema!!!

Source:Women of Christ

Reactions:

0 comments:

Post a Comment