Friday, May 31, 2013

UTASA....

Leo nataka kuongelea hili swala la utasa, jamani tunajuwa wote hata kama mnapendana kiasi gani na mkaoana ikifika wakati mmeshindwa kupata mtoto hapo ndipo ugomvi mkubwa na hata kuachana kunapojitokeza, ila kwa wapendanao wachache sana wanaopendana kwa kweli na kwa moyo mmoja huwa wanavumiliana na kutafuta njia mbadala tena wakifichiana aibu.

Nakumbuka nina baba yangu mdogo mmoja yeye na mkewe walioana na kukaa miaka 14 bila mtoto maneno yalikuwa mwengi sana kwenye familia lakini yule baba katu hakusikiliza maneno ya mtu aliendelea kuwa na kumtumikia mkewe kwa moyo mmoja wakiomba MUNGU siku awape mtoto ndipo mwaka wa 14 ya ndoa yao wakapata mtoto mmoja.

Naingia kwenye biblia sasa tunaona ya kwamba mke wa Ibrahimu hakubahatika kupata mtoto kwa muda mrefu mpaka alipokuwa na miaka 80 na hivyohivyo Isaka mtoto wa Ibrahimu alipomuoa Rebeka walikaa muda mrefu bila kupata mtoto lakini hawakukata tamaa walimuomba MUNGU naye akawapa mtoto.

Utasa unaweza ukawa umerithiwa katika ukoo kuna koo nyengine hawana vizazi vingi utakuta wamezaa watoto wachache sana na wengine hawana watoto kabisa, wewe baba ukikuta mkeo hana ama hapati mtoto kwa muda mrefu kuliko uanze kumuandama na ndugu zako ama kwenda kuzaa nje hebu tafakari ule upendo mliokuwa nao mwanzo, na tafakari MUNGU alivyokubariki ukapata mke au unadhani maujuzi yako tu ndio yamekupa mke kwani kabla hujaoa siulikuwa na wanawake wengine mbona hukuoa hao bali huyo uliyenaye ndio chaguo lako MUNGU alilokupa.

Basi tumuheshimu na kuzidi kumuomba atakupa baraka za watoto, wakati wa kipindi kigumu mnachopitia kwenye familia upendo wa ukweli mliokuwa nao kwenu ndio utawasaidia kuvuka majaribu, ila unapogeuka na kumchukulia mwenzako poa poa inaweza kuharibu kila mpango katika maisha yako na hata usielewe na kuona umhumu wa kwanini ulioa.

Tafakari

Reactions:

0 comments:

Post a Comment