Monday, May 27, 2013

Roho Imeniuma...Mmhhh

Kuna dada mmoja alikuwa ameolewa na wakazaa watoto wawili kwa umri huyu mkubwa anamiaka mitano na mwengine mitatu, kama tunavyojuwa hizi ndoa zinamapito yake na hao kwenye ndoa yao pia walikuwa na mapito ila kwasababu moja ama nyengine hawakuweza kuvumiliana wakaamua kwamba watengane, basi kila mtu akachukuwa hamsini zake.

Yule mama yeye ni mfanya biashara tu ila yule baba anafanya kazi katika bank moja hivi hapa mjini, tokea wameachana yule baba hajawahi kuwaona wala kuwahudumia watoto wake, lakini uzuzri ni kwamba mkewe alikuwa mfanyabiashara japo hakupata faida kubwa ila hakushindwa kuwatunza watoto wake.

Kuna wakati yule mama biashara zake zikawa zinamatatizo hakuwa na hela tena za kujimudu mpaka akafukuzwa kwenye nyumba ambayao alikuwa anakaa na kumuomba rafiki yake akae naye kwa muda ili ajipange, rafiki yake tunakaa naye mabibo ambaye pia nirafiki yangu basi yule mama akaja na watoto wake wakaishi tu vizuri na rafiki yake ambaye huyu rafiki yake yeye ameolewa na ana watoto wawili pia.

Wameishi kwakweli kwa amani na upendo mda wote, lakini huyu mama bado alikuwa na mawazo sana na mumewe kwakuwa alikuwa anampenda bado basi siku zikazidi kwenda lakini baadaye yule mama akaumwa ghafla ugonjwa ukamsababishia sehemu zake nyengine za mwili kufa yaani kuanzia kwenye kiuno kwenda chini pakafa.

Kwakweli nimesikitika sana basi rafiki yake naye alimsaidia sana kumuuguza huyo dada ikaendelea ya kwamba yule mama alizidi kuumwa ikabidi asafirishwe kwa kaka yake ambaye ameoa ili wamuuguze wakamuuguza kwa muda kama miezi miwili lakini yule mke wa kaka yake akaanza kuleta jeuri kwamba hamtaki wifi yake pale ni bora apelekwe kijijini kwa mama yao akauguzwe huko yeye amechoka kumuuguza, kaka yake hakuweza kabisa kumfukuza mdogo wake basi mkewe akamshauri kwakuwa pale kodi inaisha ndani ya miezi miwili basi tutafute nyumba nyengine tumuache hapo huyo dada mpaka kodi ikiisha..ukitaka kujuwa wanawake ni nyoka kweli mumewe akamsikiliza wakaondoka wakamuacha yule dada pale bila msaada wowote.

Mpaka kodi inaisha yule mama alikuwa anaunga unga maisha siku nyengine kaka yake aje amletee msaada siku nyengine hampi anajikokota hivyohivyo afanye kazi zake na MUNGU alikuwa anamsaidia anaweza kupika chakula wakala, akaweza kuwaogesha watoto aliamua kujifunza kwakuwa alijuwa itamchukuwa muda sana kupona ilibidi ajikubali ili aweze kutunza watoto wake.

Mwenye nyumba akaja kudai nyumba yake yule kaka yake akaamua kumchukuwa mdogo wake na watoto wake na kuwapeleka kijijini kwao akauguzwe na mama yao ambaye ni mzee hata yeye anahitaji msaada wa kuangaliwa, lakini kama tunavyojuwa mama ni mama alihangaika kumuuguza mwanye pamoja na watoto wa mwanaye huku yule mama akijitahidi hivyohivyo kuishi maisha yake akiwa nusu hai.

Majaribu haya jamani, siku moja yule mama akaumwa ghafla homa kali na kutapika ikabidi mama yake atafute msaada kwa majirani wampeleke hospital wakampeleka akapimwa na kugundulika ana malaria na uti basi kurudi nyumbani na ile hali aliyokuwa naye na kuumwa tena akawa hoi mpaka mama yake akaanza kushindwa kumuuguza maana hakuweza hata kushuka kitandani.

Akawa ni mtu tu wa kulala kitandani malaria ilimdhoofisha sana, lakini MUNGU bwana sio mwanadamu akapita kijana siku moja kuulizia njia kwenye ile nyumba ndipo alipogonga na kukaribishwa ndani maana yule mama alikuwa anamlisha mwanye ndani watoto wakamwambia kwamba wapo ndani pita akamkuta yule mama anaumwa akiuguzwa na mama yake ambaye ni mzee roho ilimuuma sana na akamuomba mama awe anamuuguza yule mdada..yani mtu ulitaka kuelekezwa njia akaishia kuwa msaada mkuu huyu MUNGU jamani.

Basi kijana akawa anatoka kwao mbali na hapo anakuja kwa mwanamke kumuuguza kila siku uguza uguza na wewe lakini kwa mpango wa MUNGU yule mama akafa, yule kijana aliumia sana kama alikuwa anamjuwa tokea mwanzo basi taratibu za kumzika zikaanza kufanyika, ikabidi wamtafute baba watoto wake wampe habari yule baba akawajibu kwamba yupo njiani anaenda safari hawezi kuja wamzike tu..mmhh watu waliumia kweli mtu ni mkeo na amekuzalia watoto mmetengana ndio leo huoni umuhimu wake.

Watu na ndugu wakafanya msiba na kuuzika mwili siku ya tatu wanampigia yule baba kuhusu watoto wake anasema hawezi kuja kuwachukuwa watafutiwe sehemu wakae, basi kuna kaka mmoja ambaye alikuwa ni mjomba wa marehemu akasema basi yeye angewachukuwa mkewe akakasirika sana na kumwambia kama utawachukuwa utafute na housegirl wa kuwaangalia maana yeye hana huo muda!!!!!

Mpaka tunapewa hizi habari wale watoto walikuwa kwa bibi yao, yani roho inaniuma mimi haswa kwakuwa nilikuwa na mjuwa alikuwa mdada mzuri ana roho nzuri, inaniuma sana kwakuwa yani mtu hata kama mmeachana huoni umuhimu wa watoto wako ugomvi wako na mke wako unawahusu nini watoto wataishia mitaani wewe ukila raha,halafu sisi wanawake yani mwanamke unakuwa huna huruma na mtoto wa mwanamke mwenzio kweli unakataa kumtunza unaona mzigo wewe unajuwa kesho yakikukuta atakutunza nani mumeo?? wakati tena unaweza kuta mwanaume ukiumwa yeye ndio kapata visa ya kutoka nje na kustarehe, ni wanaume wachache sana utaumwa akuuguze kwa upendo na ukweli mpaka upone, mwanamke unakuwa huna huruma na watoto ambao hawajakukosea kitu, jamani wanawake tujifunze.

Ukishakuwa mwanamke MUNGU amekupa sense ya sita ya ziada ni kuwa na moyo wa chuma, mangapi tunafanyiwa mabaya lakini bado tupo pamoja na kulea familia zetu lakini mwanaume akitikiswa kidogo tu na mkewe na nyumba ana hama na anatafuta mahawara kumi wa kumtoa mawazo..ukishakuwa na kujijuwa wewe ni mwanamke lazima ujuwe unajukumu la kujitunza wewe na jamii nzima ni jukumu lako kusaidia pale unapoweza hata kwa mawazo tu ndio maana wanasema ukielimisha mwanamke unaelimisha jamii sasa wanawake wasikuhizi ni wabinafsi, wachoyo, wanafki jamani...tujirekebishe kwakweli fanya mema na MUNGU atakulipa usisubiri kulipwa na binadamu maana utasubiri sana.


0 comments:

Post a Comment