Monday, May 27, 2013

I love me some Sheria Ngowi........designs

Leo nilikuwa napitia blog ya 8020 kama kawaida yangu i love this blog na mwenye nayo amenisaidia mengi sana na ananifunza mengi pia..so nikaona hii picha nikagundua kumbe wanaume wengi hupendeza sana wakivaa suits it doesnt matter utaivaa ipi na rangi gani ila hichi kitu bwana hakimkatai mtu..wamevaa vijana wamependeza

Kwa wanaume ambao mnapenda kujichukulia poapoa i have an advice for you wanawake wengi wanapenda wanaume wanaojuwa kuvaa na kujitunza aihusu ukatembea barabarani na mkeo/girlfriend wako ukaanza kusalimiwa kwa heshima ukidhaniwa baba yake mdogo kwa jinsi ulivyoozeeka na mavazi yako..

Wanawake wengi ukimtongoza cha kwanza anaangalia muonekano wako wa nje halafu mengine hufwata baadaye baada ya kukubaliwa, kama mimi nakumbuka enzi za ujana (kabla sijaolewa) mwanaume alikuwa akinitongoza cha kwanza kumwangalia ilikuwa ni viatu, then nguo maana kama huwezi kutunza viatu vyako vinavyokustiri miguu uweze kujitunza utaweza kunitunza miye...nikikuta kimejikunja na kuzeeka jibu ni hapana kabla hata hujaanza sentensi ya pili..

Kwahiyo kwenu wanaume looking sharp ndio habari ya mjini, japo kuwa siku hizi wanawake wengi tunapenda hela kuliko kitu chochote, ngoja niwachekeshe kuna kipindi cha nyuma nilikuwa na marafiki zangu wa kike watatu tukawa sehemu tunazogoa mwenzetu mmoja akasema kwamba ametongozwa na mwanaume sio mzuri ni wa kawaida sana yani hawezi hata kukubali kuolewa naye akimuomba ila tu kwa sababu ana hela zake za haja ndio maana anakuwa naye kwakuwa anamuhonga hatari, sasa mimi kama mnavyonijuwa kwa mdomo nikamuuliza sasa kama anasura mbaya mkiwa kwenye mzunguko inakuwaje humuangalii usoni hahahaha akaniambia wakiwa wapo mafichoni mwao huwa anapokuwa kwenye mzunguko anapenda awekwe style upande atakayoona suruali kwani anajuwa mule kuna hela za kupewa akimalizana na bwana kwahiyo yeye akiwa anazunguka anaiangalia tu ile suruali upande wa wallet..hahahahaha mji huu unahatariiii.

 Nikamwambia sasa inamaana gani kujipa adhabu unazungushwa na mtu humpendi basi bora uwe humpendi kwa muda huo lakini moyoni unajipa moyo utampenda baadaye unatumia nguvu zako huku haufurahii kwasababu ya pesa akaniambia bibi wee kwani sura yake natembea nayo mfukoni sinamuachia mwenyewe cha muhimu ananihudumia basi...hatareeeeee

Hicho ni kibonzo cha leo kwenu nyie wanaume mvuto ni  muhimu kwa maisha haya ya sasa... 


Reactions:

0 comments:

Post a Comment