Tuesday, May 28, 2013

Mapito ya ndoa na Mashoga....

Leo nataka niongelee kitu kimoja ambacho nimeona ndoa nyingi sana zikiingia matatizoni na wengine kuachana kwa sababu ya huu uzembe na ndio maana napenda sana kuukazia.

Jamani mashoga ni wazuri sana na nikiongelea mashoga ni marafiki wa karibu wa kike, wengi tunao na wengi pia bila hao mashoga wasingefika mahali walipo, kuna mazuri mengi ambayo mashoga wanaweza kukufanyia na mabaya mengi ambayo pia wanaweza kukufanyia, na hapa nataka na wanaume pia wajifunze kwa marafiki zao wakaribu.

Kabla hujaolewa unakuwa nao wengi sana lakini umeshagundua kwanini wanawake wengi wakishaolewa huwa hawana kabisa mashoga??? sio tu kwasababu wapo busy na familia zao bali hawaoni tena maana yakuendeleza ama kuuweka ushoga mbele kuliko familia zao.

Nasio vizuri kwa mwanamke uliyeolewa ukapata matatizo na mapito katika ndoa yako na ukayapeleka kwa wazazi wako au hata ndugu zako kwani unajenga uwadui wao kumchukia mumeo kwani nani ambaye anapenda mtoto wake apate tabu lazima watakasirika na kumuona mume hana maana, ndio maana napenda kushauri wanawake kwenye ndoa kuwa na mashoga ambao na wao wanandoa ili waweze kutoana mawazo na kupeana nguvu ya kuendelea na ndoa, maana ndoa jamani sio mchezo wa kuigiza kwamba ukicheza hivi leo kesho mnaweza kufuta hicho kipande kwenye script na muweke kingine..ohoooo

Narudia tena muelewe sikatazi mwanamke aliyeolewa kuwa na mashoga ambao hawajaolewa maana kuna vitu kama upatu mnaweza kucheza pamoja kwa ajili ya maendeleo kuna wakati mwengine mnataka tu kutoka muende sehemu muongee na kufurahi, ila kwanini napenda kushauri wanawake walioolewa kuwa na mashoga wengi ambao na wao wameolewa na kutokubali kuwa na mashoga wengi ambao hawajaolewa ni kwasababu zifwatazo.

Kwanza kabisa wote tulio kwenye ndoa tunajuwa mapito ya ndoa yalivyo mengi na kila mtu anapitia hakuna mtu yoyote ambaye yeye ndoa yake ni tambarale tu siku zote ila tu mapito yetu yametofautiana, sasa bas labda wewe mama kwenye ndoa yako mumeo ni mlevi hatari anarudi usiku wa manane amelewa, hela ya matumizi nyumbani haachi anakuambia hana akirudi yupo tilalila umeshamsema na kumshauri lakini habadiliki utafanyaje hapo ndio unamuhitaji rafiki yako fulani mwenye ndoa akufahamishe cha kufanya maana kama yeye halalipitia hilo basi kapitia kitu karibu na hicho na yeye si ana ndoa, sasa wewe kampelekee yule shoga yako anayekula na kulala kwa mama uone atakalokujibu cha kufanya ni wachache sana wenye busara, juzi nimesikia msemo ukimwaga ugali nitamwaga mboga..utafakari kiutu uzima.

huo ni mfano tu ambao utakusaidia kuelewa kwanini huwa napenda kushauri wanawake walioolewa kuwa na mashoga zaidi ambao na wao wameolewa.

NOTE: kwa upande wangu mimi siwezi kumuomba ushauri wa ndoa shoga yangu aliyeachika kwenye ndoa kwakweli siwezi maana kama yeye kashindwa kumudu maumivu ya ndoa atanishauri nini mimi, labda kama ameachika kwenye ndoa kwasababu za kueleweka labda mumewe malaya sana harekebishiki na kashindwa kuvumilia, au mwanaume hana muda na familia yake akaona bora alee watoto wake mwenyewe na sababu nyengine ambazo zinaeleweka, lakini sio mwanaume kachelewa kurudi mara mbili ukalianzisha timbwili na kuondoka..akuuuuu sitaki mawazo yako mimi.

Kama limekuchoma shoga utanisamehe ila ukweli wangu ndio huo...


5 comments:

  1. Tutaongelea haya yote na mengine tukikutana kwenye mafundo ya wanawake walioolewa, sasa hivi ninachanganya mafundo ya chumbani na mengine ya ndoa kwa ujumla..ili tuwekane sawa maana wengine wanamatatizo zaidi kwenye maisha ya ndoa kuliko maisha ya chumbani kwenye kitanda cha ndoa..

    ReplyDelete
  2. Its a nice advice keep goin sis! We i was in tanzania i cud have come to ur session of marriage issues! Do you make a movie so dat i can get ur lessons? Plz reply n thanx in advance

    ReplyDelete
  3. Ujumbe mzuri sana.

    ReplyDelete
  4. Ujumbe mzuri sana. Ila weng tunashndwa kuchangia mada zako kwasababu ya usumbufu wa hapo penye...prove that u r not a robot... Tunaomba upaondoe hapo kwani tunaotumia simu panatusumbua, so, huwa tunakuja tunasoma lakin hatuchangii

    ReplyDelete
  5. kweli bhana hiyo process ya prove inasumbuaga hadi ina kera

    ReplyDelete