Wamama wa miaka ya sasa tupo busy sana hasa wa mijini. Unaondoka nyumbani bado giza, unatoka kazini unapitia kwenye ujasiriamali au shule, ukifika nyumbani watoto wamelala au hata ukikuta hawajalala umechoka huwezi hata kuzungumza nao. Maisha ndivyo yalivyo na hatuwezi kubadilisha hilo. Ila unaweza kuamua kujipanga vizuri, siku ambazo huendi kazini zinakuwa ni maalumu kwa ajili ya familia.
Usikae mwezi mzima hujamwogesha mtoto wako wa chini ya miaka mitano, kumwogesha na kumvalisha sio tu kutakufanya uwe karibu zaidi naye, bali kama kuna tatizo kny ngozi yake utagundua. Weka ratiba kuwa kila weekend wewe ndio utakuwa unawaogesha watoto. Pia wapikie chakula wanachokipenda angalau mara moja kwa wiki. Inapendeza pale watoto na mume wanapojua kuwa chakula fulani the best cook ni mama.
Pia ukiwa nyumbani jishughulishe na watoto wako, sio mtoto anajisadia wewe upo naye unamwita dada aje ambadilishe, ni mwanao, be proud to take care of him/her.
Source: Women of Christ
0 comments:
Post a Comment