Wednesday, April 17, 2013

Nivumilieni mwenzenu..

Jamani wapendwa nipo busy nazungusha madera na kukutana na wadau wangu live kuongelea mawili matatu kuhusu shughuli yetu ndio maana mnaona kimya na mtaani sipo kabisa ndio maana sijawaletea story za mtaani kwetu..ila nimekumbuka kuna moja ya juzi nilivyokuwa nimerudi..mmmhhh shoga umbea huu nitasutwa anyways ilikuwa hivi..

Kuna mdada mtaani kwetu ameolewa mwaka jana mwezi wa tisa, masikini huyu dada kila akibeba mimba ikifika miezi sita inatoka, kwa story za hapa na pale za mtaani ni kwamba yule mumewe kabla hajamuoa alikuwa na mwanamke wake ambaye alimpa mimba na kumuacha ndio akamuoa huyu mwengine kwahiyo yale machungu ya yule mwanamke wa kwanza ndio malipizo yake ndio hayo au kamloga asibebe mimba ndio maana kila zikifika miezi sita zinatoka...

Wengine wanasema kwamba inaelekea huyu dada alikuwa anatoa sana mimba kabla ya ndoa kwahiyo kizazi kimelegea mtoto anapofikia miezi sita akiwezi kuhimili uzito kwahiyo mimba inatoka..

Sitakaa kusahau maana niliona mwenyewe mtoto alivyotoka, wamama watu wazima wakaenda kumzalisha ndio baadae akaenda hospital, mumewe kurudi jamani wala hakupapatika kwamba mkewe yupo hospital amfwate akamuuguze wala ndio kwanza akakaa kijiweni na wanaume wenziye na kutia story mpaka usiku na akalala kwa amani mpaka asubuhi bila hata kumuona mkewe!!!!!ndoa haina hata mwaka

Mmmhh wanaume hawa!!!! anyways hizo ndio za uswahilini kwetu mabibo, nikiwa na mpya nitawaletea ila simnajuwa event yetu ni wiki ijayo 26/4/2013 kwahiyo nakimbizana na maandalizi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment