Tuesday, April 30, 2013

Mwanamke na Ndoa yako...

Wapendwa tarehe 5/7/2013  tutakuwa na mafundo special kwa wanawake walio ndani ya ndoa tu na naomba please kama sio mwanamke mwenye ndoa usidanganye ili kuingia humu yatafanyikia palepale Majestic hall Sinza kwa Remmy 10:jioni-5:usiku hata kama unashughuli usiku huo pitia pale kidogo hata kwa masaa mawili tu halafu uondoke sikushauri ukose, kiingilio 30,000/= mje mmevaa comfortable maana tutakaa chini kwenye mazulia hiyo ndio style ya wafundwaji inaonyesha unyenyekevu.

Kwanini nasema hivi mafundo haya ni tutaongelea kiundani zaidi kuhusu ndoa zetu kuna wanawake ambao wanamatatizo sana kwenye ndoa zao au changamoto ni kubwa sana katika ndoa zao sasa wewe ukaingia humu na huna ndoa utatamani tena ndoa kweli ama ndio utajipe mapresha lakini wote ambao tunandoa naamini kwa namna moja ama nyengine wote hayo matatizo ya ndoa tumeshayapitia ama tunaendelea kuyapitia.

Wanawake wenye ndoa zao pia watafundwa nini maana ya uke na jinsi ya kuutengeneza na kuuimarisha watafundwa kuhusu wame zao na miili yao na afya zao, kutakuwa pia na watu ambao wataonyesha jinsi wanavyoweza kujimudu na miili yao wakiwa chumbani na watu hawa ni wake za watu yani siku hii kila kitu kwanzia burudani mpaka watoa mada ni wake za watu.

Najuwa na kuamini kazi yangu mnaikubali watakuwepo makungwi wakongwe watu wazima wanaojuwa kukufunda kuhusu ndoa yako wakakuchambulia ndoa wakakupa majibu ambayo wewe kwa umri wako huna na labda hukudhani kama utayapata cha muhimu ninachoomba kwa watakaolipia na kuja ni kwamba kuwa wawazi msiogope kuuliza maswali na hata kama unahisi kuogopa niandikie kwenye karatasi nitawaulizia.

Tutafundwa, tutajifunza tutamwaga stress zetu, tutakula na kunywa tutatoka hapo wepesi tayari kwakuendeleza safari zetu za ndoa..

Naamini hakunaga kuachika mtu hapa kwenye ndoa wewe unifanye mimi niachike kwenye ndoa unanini la maana au lakunizidi mpaka unitoe kwenye nyumba yangu, labda kama umefundwa na mimi sijafundwa lakini vinginevyo huna jeuri hiyo.

Huwa napenda kuwaambia wanamwake ukiwa kwenye ndoa lazima uwe mbunifu na kutaka kujifunza mapya kuhusu ndoa yako ndoa sio nywele kila mtu anayo kunawanawake wazuri kwa mwili na akili shoga lakini hawana ndoa kila kukicha kudandia waume za watu maana wao sio wa kuoelwa lakini wewe unayo unaichezea endelea kubweteka shoga yangu wenye mafundo yao wakufundishe adabu.

Tukutane siku hiyo naitangaza mapema ili mjiandae isiwe kama iliyopita watu wanasikia siku za mwisho wakati tickets zilishaisha, ukiisoma hii mwambie na shoga yako..

2 comments:

  1. Hapo kwenye muda ni mtihani kwa wengine kupata ruhusa kwa waume kukaa mpaka usiku. Nashauri ubadilishe muda iwe during day timebadala jioni ili tunaokaa mbagala tuje mapema turudi kwa waume zetu mapema pia. Naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  2. Wengi wetu tunapenda kuhudhuria ila muda unatubana, nadhani unafahamu kupata visa ya usiku kwa mke wa mtu ni ngumu hivyo nakuomba ufanye mabadiliko katika hilo ili wengi tuhudhurie, la hasha watakuja wavamiaji c walengwa

    ReplyDelete