Tuesday, March 19, 2013

Wanaume wafujaji...

Jamani wanawake haswa nyie ambao bado hamjaingia kwenye ndoa mnaolilia na kutamani ndoa kila siku kabla hujatamani kuingia kwenye hiyo ndoa unamjuwa vizuri huyo mwanaume maana bwana kuna wanaume wengine hodari kweli kuficha makucha yao mpaka baada ya ndoa ndio unaanza kupatwa ugonjwa wa moyo ka maudhi yao.

Jamani wanawae kuna wanaume wafujaji yani hawa wanaume wao wana kero kwao kila kitu majanga mwanaume ndani amani hakuna mwanaume hakupi matumizi mwanaume tena wengine mpaka kazi wanakuachisha, utamkuta mwanaume anajiweza ana hela anamagari lakini kuliko akupe wewe gari bora alione limepaki kwake akiamka afurahi kuhesabu idadi aliyonayo basi tu kukuchakaza wewe..inahusu

Mwanaume tena mwengine unaishi naye lakini hata hujuwi anachokifanya nini ukimuuliza jibu ni kwamba wewe hela ya matumizi sinakupa sasa unataka kujuwa nini hilo ni sawa bora useme ili kama jambazi niishi nikijuwa wewe jambazi siku polisi wakija kutushika pindo za nguo tujiandae.

Mwanaume kutwa nyumbani waje ndugu zake yeye tu tena wakae wanavyotaka wakija ndugu zako utaanza kusikia maneno mara akuulize wanaondoka lini jamani yani wewe ndugu zako sio kwao pale bali ndugu zake yeye tu, tena utamkuta kila anachoambiwa na ndugu zake yeye anakubali kufanya lakini wewe mkewe hata umwambie unashida ya hela ya kufanya kitu cha muhimu atakuzungusha na visingizio kibao..inahusu

Mwanaume mwengie tena kwakuwa ndugu zake ndio wanaishi pale maneno na majungu yakitokea kutwa wewe unasingiziwa ubaya na ndugu zake hata kufanya utafiti hafanyi yeye kugombana na wewe tu na kukunyima usingizi kisa cha kumzeesha mtoto wa mwanaume mwenzio ni nini kisa umeoa inahusu...

Jamani maisha ya ndoa tunategemeana mume na mke tabia za kujifanya wewe ndio wewe uifanyie huko nyumbani kwa wazazi wako au ulipopanga kabla hujaoa siku hizi wanawake wanajitambua na ndio maana na kufunda pia tunafundana kujuzana zaidi hakuna anyetaka kuonewa kisa mapenzi kila mtu kaumbiwa mpenzi wake hata paka naye anaye mpenzi kwahiyo tusichukuliane poapoa kama vipi utatupwa huko kwenye dustbin labda takataka ndio size yako. Mixxxuuuuuuuuuuuuuuuuu

Reactions:

0 comments:

Post a Comment