Monday, March 4, 2013

WALOKOLE...

Tena na hili leo nataka niliongelee haswa liwafikie nyie mliookoka, jamani kuokoa ni mtu binafsi na maisha yake labda na familia yake, kinachoniudhi mimi ni walokole wengine tena kutaka kujifanya wao ndio ulokole umewakolea mpaka kwenye nanihiiiii...

Kama unajuwa wewe mwanamke/mwanaume umeokoka uushike ulokole wako inavyotakiwa na ukiamua kuwa na girlfriend jitahidi kuzuia tamaa za mwili inatakiwa mkishaoana ndio muanze kuchuma tunda sio wewe tena ndio ushamuona binti kidawa mtoto ana ushepu akipita anajitingisha upande kama dera tamaa ikakushika unajikuta unachuma naye tunda kabla ya ndoa.

Jamani shetani bwana anajuwa mwisho wa kiburi cha mwanume kitandani siye wanawake tunaweza kujikaza lakini mwanaume akiuona sketi tu nanihii kashasimama..halooooooo na ndio kama wewe umeokoka ukaenda kutongoza ambaye hajaokoka basi kazi ndio unayo maana yule yeye dozi kutwa mara tatu wewe ukampe noo inahusu atakaa uandhani ama wewe ndio utaheshimiwa maana unaweza kumuoa halafu atatafutwa wapembeni wa kumalizia shida zake..labda kama anajiheshimu na kukupenda kwa ukweli

Tatu hii iwaendee wanawake wote walioolewa halafu ndio wakaja kuokoka, tena ngoja nikae vizuri kuandika hii..shoga inahusu nini kama wewe leo umeamua kuokoka halafu hutaki kumpa mumeo tunda kisa yeye hajaokoka Inahusu????

Tena utamkuta mwengine na chumba anahama..enhee endelea halafu baada ya muda unaanza kulia na MUNGU ndoa yako haina amani inavunjika mwanaume kutwa anarudi usiku, mara hata nyumbani hali sasa unategemea awahi kurudi akumbatie mto ama huo mto ndio unamaliza shida zake za tunda..shoga tena na hivi hajaokoka akikutana na wanawake wa mjini wanaojuwa kuzungusha kiuno na nyumba atahama nini kuchelewa kurudi..kama unatabia hii jirekebishe na kama kanisa lenu ndio likauambia hivyo hama

Kama umeokona ma mume/mkeo hajaokoka endelea kuishi naye kama zamani mpe mzigo kama kawa huku ukibadilisha vitu taratibu na kumuomba MUNGU ambadilishe naye baadaye atabadilika usitake kulazimisha mambo kisa wewe umebadilisha kuabudu mwanamme ana nembo "hold with care" anataka kubembelezwa na kulelewa kama mtoto sasa wewe jifanye mama yake unataka kumtia discipline utaisoma junejuly.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment