Tuesday, March 5, 2013

Kweli kabisa na hili ndio tatizo la ndoa nyingi kuvunjika na nyingi zikiwa changa..

ZAB. 127:1
BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.

Mungu pekee ndiye anayeweza kumlinda mume au mke wako. Kuhangaika kuchunguza simu kila akiiweka pembeni, kuangalia emails, kumfuatilia kila anapoenda na kumwekea watu wa kumfuatilia haitakusaidia kumlinda. Mkabidhi Bwana, mfunike mwenzi wako kwa damu ya Yesu na amini kuwa yeye ndiye mlinzi pekee.

Usitafute ugonjwa wa moyo kwa kuhisi hisi kila anapoongea na simu, mkabidhi mikononi mwa Mungu nawe uishi kwa amani.
 
Source: Women of Christ

Reactions:

0 comments:

Post a Comment