Thursday, March 21, 2013

MWANAMKE MMOJA WAUME WATANO, WOTE NDUGU, KILA MMOJA ZAMU YAKE KWENYE CHUMBA KIMOJA

               Rajo na familia yake wakiwa mbele ya kibanda chao chenye chumba kimoja.MWANAMKE, Rajo Verma, 21,  mkazi wa mjini Dehradun, India, anaishi na wanaume wake watano katika kibanda chenye chumba kimoja ambapo hulala na mwanamme mmoja kila usiku. Mwanamke huyo hana uhakika na baba wa mtoto wake mdogo wa kiume ambapo anasema: 
“Mwanzoni niliona matatizo kuwahudumia wote katika kuwapa unyumba. Lakini sasa nawahudumia wote bila upendeleo.”
Mumewe mmoja aitwaye Guddu, 21,  ambaye alikuwa wa kwanza kumwoa anasisitiza: “Wote tunafanya naye tendo la ndoa bila wivu.  Sisi sote ni familia moja yenye furaha.  
Jamaa huyo alimwoa Rajo miaka minne katika ndoa ya mila za Kihindu na ndiye mumewe halisi.
Lakini mila kijijini kwake zilimlazimu kuwachukua kaka za mumewe pia kama waume zake. Hao ni Bajju, 32,  Sant Ram, 28,  Gopal, 26, na Dinesh – ambaye alimwoa kwa njia hiyo ya kimila mwaka jana alipofikisha umri wa miaka 18.
Bajju ambaye ndiye mkubwa kuliko wote anasema: “Namchukulia kama mke wangu na ninalala naye kama wanavyofanya ndugu zangu.” 
Rajo anafanya kazi zote za nyumbani na kumtunza mtoto wake aitwaye Jay, mwenye umri wa miezi 18, ambapo waume zake huenda kufanya kazi kila siku mjini Dehradun.
Mwanamke huyo anasema mama yake pia aliwahi kuolewa na ndugu watatu wa kiume, hivyo hilo si jambo la ajabu kwake.
“Ninalala nao kwa zamu. Hatuna vitanda chumbani bali tunatumia mablanketi yaliyotandikwa sakafuni. Watu hao hunijali na kunipenda zaidi, jambo ambalo wanawake wengi zaidi hawalipati katika ndoa zao,” anasema.


Chanzo:Global Publishers

3 comments:

  1. kazi kwelikweli hawa wana habari kuwa ukimwi upo kweli?duuu!mila kama hizi hazifsi ktk dunia ya leo

    ReplyDelete
  2. Satan is Liar eeh mwenyezi mungu Rudi upesi tunaangamia yale yaliotendeka Sodoma na Gomora ndio yatendeka sasa.

    ReplyDelete