Sunday, March 24, 2013

Muhogo...chezea wewe

Wanaume wengi wa kitanga, wapemba, wa lindi na wazaramu wanapenda sana kula muhogo lakini hawa wanaume bwana wa sijui wapi labda ni kwavile hawajui umuhimu wa muhogo au hata kama wanajuwa labda hawawezi kwenda sokoni kununua au hawezi kuwaambia wake zao wawape muhogo kwani hawataki kuhojiwa mengi.

Lakini kwako mwanamke unajuwa faida za kula muhogo ama shoga ndio mpaka uwe na hamu umuambie mpenzi muende coco ukale hapana unatakiwa usiukose kabisa ndani kwako na sio lazima mpenzi wako ajuwe unampa muhogo kunanjia nyingi sana za kuuweka muhogo bila yeye kujuwa ila ukawa unamsaidia mengi tu ikija kwenye afya yake.

Na ninajuwa wanawake wengi hawajui muhogo unatibu nini, watautengenezaje maana tiba yake ni nzuri muhogo ukiwa mbichi na sio wa kupika sasa kama wewe mwanamke unataka kujuwa unatibu nini na jinsi gani utampa mpenzi wako bila yeye kujuwa kama haupendi kula mbichi utampaje...

Usikose 26/4/2013 katika mafundo lipia nafasi yako mapemaaaaa

Reactions:

0 comments:

Post a Comment