Tuesday, March 12, 2013

Msaada Tutani..

hello dada Rose  habari za kazi pole kwa shughuli za kuelimisha jamii mimi nimekuwa  mtumiaji mzuri wa website yako nikiwa nafuatilia habari na matukio  ktika website yako ambayo kwa kiasi kiikubwa inatuelimisha na kutujuza mambo mambalimbali!
 
   mimi ni kijana  wa kiume wa miaka 29 nina tatizo moja limejitokeza kenye sehemu za siri za nyumba ,(mk***ni) kwa maeneo ya nje .ni uvimbe ulio toa kinyama mithili ya jipu  nilienda hospitalini wakanipa dawa za kuingiziza  mk********ni na vidonge vidogo vya kumeza  pamoja na dawa ya kupaka but  kilicho tokea ni kwamba maumivu makali yameisha ila uvimbe uko pale pale  nimejaribu kufuatilia kwa ukaribu kwenye mitandao nikagundua ugonjwa wenyewe waitwa  
 
Hemorrhoids  unao sababiswa na vitu vingi vikiwemo kutopata choo cha mara kwa mara au choo kuwa kigumu, kunyanyua vitu vizito au kazi ngumu,kuharisha kwa muda mrefu etc,
    hivyo nlikuwa naomba  unisaidia kama kunatiba ya asili  coz  nimesikia mahala kuwa kitunguu swaumu ni dawa ila sijui kinachanganywa na nini !plz mwenye naomba msaada weko!
 
 
 asante  kwa yote Mungu awabariki!

5 comments:

  1. Hello

    Pole sana kwa tatizo hilo sijawahi kulisikia kabisa ila nimetuma kwenye blog wengine wakusaidie pia lakini kama dawa umeambiwa ni mafuta ya vitunguu swaumu mimi huwa ninayo hayo mafuta ila sijui kwa huo ugonjwa utatumiaje kwa dawa za asili sijui kwakweli.

    ReplyDelete
  2. kijana mwenye matatizo pole sana mimi ninachokushauri ni kwamba endelea kuwaona wataalam mapema yaani uwende tena hospitali kwa wataalamu wa juu maana hilo tatizo sio ndogo na ukiendelea kukaa utakuja kupata shida zaidi ulizia zaidi madactari wanaoshuhulika ma maeneo hayo usiona haya ktk ugonjwa kwani mficha maradhi kilio kitamfichua rudi tena hospitalini wachukue vipimo

    ReplyDelete
  3. Kaka nimeongea na watu wazima nikawaambia kuhusu huo ugonjwa wakaniambia dawa yake ni majani ya mnyonyo unayachemsha halafu unayaacha yawe ya uvuguvugu unaweka kwenye beseni unakalia yasiwe maji mengi mpaka dawa ikayeyuka yawe tu ya kutosha ile rangi ya majani iwepo unayakalia kwa muda wa nusu saa mpaka lisaa lizima mara mbili au tatu kwa siku fanya hivyo kwa muda hata wa mwezi.. wananiambia kuna mtoto naye alishapata huo ugonjwa hayo majani ndio yakamponesha natumaini na wewe yatakufanyia vyema usiache na kumuomba MUNGU akusaidie maana yeye ndio mponyaji mkuu

    ReplyDelete
  4. pole sana mwenye tatizo. kuna dawa ipo ya kuchoma huko kwenye hivyo vinyama , ipo kama lipshine umbile lake, unachoma kila siku asubuhi na jioni

    ReplyDelete
  5. mimi ni msichana ambaye nina tatzo hilohilo.kiukweli hilo tatzo ni nadra sana kulimaliza na hata ukiliacha halina tatizo lolote linalokuletea kwasababu kile kinyama kinatokana na nyama ya ndani ya mk****ni kusukumwa na kitu kigumu na kutoka nje kwahiyo hamna tiba ya kuirudisha ndani maana imeshalegea kutoka nje labda kwa kufanyiwa upereshen ya kuikata na si kupotea kimazingira so kama huna tena maumivu isikusumbue tena kuangaika nacho kwani hakidhuru chochote zaidi.

    ReplyDelete