Monday, March 18, 2013

Mahawara..

Jamani leo nataka niongee na mahawara mahawara wapo wa kila aina wanaume kwa wanawake kuna mahawara ambao wameoa/olewa ama ambao hawajaoa/olewa, ndio kwani hujaona fulani kaolewa lakini ana hawara nje ama yule baba kaoa lakini anahawara nje hivi vitu japo tunajuwa havimpendezi MUNGU lakini bado tumeamua kuvifanya.

Sasa basi leo nataka nikupashe wewe hawara tena upande wa wanawake maana najuwa wanaume hawana hizi tabia hivi wewe mwanamke unajuwa kabisa ni hawara wa bwana fulani inahusu nini unataka kujifanya wewe ndio wewe umpiku mkewe inahusu yani utakuta mtu anakazana kweli kumtia mke wa mtu ubaya tena haswa kama anamjuwa mkewe ilimradi tu achafue hali ya hewa kwenye ndoa ya mwenziye.Haipendezi

Sio uone zamu yako leo ukadhani wewe ni binti kidawa shoga wewe sio wakwanza na unaweza usiwe wa mwisho lakini mke wake hatakaa kubadilika atabaki yuleyule mpaka kifo kiwatenganishe kwahiyo myatambuwe hayo utamkuta mwanamke anajihashua tena kutafuta simu ya mkewe umpigie umrushe roho utamrusha roho nani tena kwa taarifa yenu mlio kwenye ndoa ngoja niwaambie ukiona hawara anakupigia simu ama anakutumia text kukurusha roho ujuwe huyo mbovu hana jipya katoa huko halijanoga anataka kukuharibia wala asikurushe roho.

Watu wanakula kwa malengo wote tumepitia huko usijitape sana ukajiona wewe ndio wewe ila sisi wakati hizo tulikuwa na heshima tena ikifika week end ndio humtafuti jamaa mpaka akuanze wewe kumuheshimu kwani yupo na mkewe lakini watoto wa siku hizi sijui wamekuwaje au ndio nyege zimezidi vipimo maana utakuta mtoto wa kike usiku unamtafuta mume wa watu asubuhi unaanza wewe hata tongotongo hajasafishwa na mkewe ukifanya hivyo unadhani ndio sifa tena wanaume wengine wanaonaga kero ndio maana wanazima simu zao usiku na huziwasha wakifika makazini maana hawataki waharibiwe kwa wake zao..

Watu kwenye ndoa zao hutoka nje kwa sababu nyingi tofauti, mke hutoka nje kwasababu mbili kuu kwanza mapenzi ya kipungua mume utakuta tena sijui kisingizio kazi nyumbani ukifika mapenzi hakuna huo mzunguko ndio kabisa hutoi ukitoa tena moja sasa wewe hamu imeisha mkeo je?? ndio mawazo wengi yanapoanza kuwajia kutafuta nje lakini wakifika nje kama akishapewa vizuri na hamu ikamuisha atakuwa anamtafuta hawara huyo akitaka mzunguko TU..  kwasababu hata unipende vipi siwezi kupenda mume na hawara kwa wakati  mmoja wewe mapenzi nitakayokupa ni yale ambayo mwisho wake ni kitandani ili nienjoy mzunguko wako maana huwezi enjoy mzunguko kama unafanya na mtu ambaye humpendi.

Lakini siku zote baada ya matatizo yanayofanya watu watoke nje kuisha au upepo huo kupita pindi wanandoa wanapopatana basi mapenzi kati yao huwa motomoto hata mahawara wa nje hatukumbukwi tena na hapo ndio utautambua umuhimu wako kwahiyo usipende kujishebedua ukijipamoyo wewe ni wamaana kwa manaume/mwanamke yule bali wewe ni TUMIKO tu unatumiwa unapohitajika usipohitajika unatupwa huko kwahiyo kula kwa malengo na heshima.

Tabia hii inamchukiza sana MUNGU...kwahiyo kila tunapolifanya tafakari vyema.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment