Monday, February 18, 2013

Uswahilini kwetu...

Ndugu yangu unaambiwa ukija jijini huku na jembe utalima lami, yani kuna vituko vingine vinatokea mpaka mtu sasa unashindwa kusikitika unabaki tu kucheka..

Kuna mdada mmoja amepanga chumba kimoja tu anaishi na mtoto wake huyu dada hafanyi kazi huwa tu mara nyingi tunamuona mtaani.

Sasa jana katoa kali ya mwaka kama kawaida mtu unapokuwa mtu mzima na kuamua kupanga basi tunategemea nyumbani kwako kuingia wageni wa kila aina na hakuna atakayekuuliza kwasababu wewe siumelipa kodi?

Sasa kumbe yule shoga alikuwa na wanaume/mabwana watatu mmoja polisi, dereva wa bodaboda na mwengine mkaka tu mfanyabiashara na kati ya hao wote ni wame za watu kasoro dereva bodaboda. Huyu mama anamtoto mdogo na huyo mtoto kila mwanaume hapo ni baba yake na anakadi tatu za clinic kila kadi inajina la baba tofauti.

Alikuwa anajuwa sana kuwapanga hawa wanaume lakini kama ninavyowaambia kila siku ipo siku wewe unayesaliti ndoa yako utailipia kabla ya kuonja umauti.. kwanzia majuzi mtoto alikuwa anaumwa na shosti akamwambia kila mwanaume kwamba mtoto anaumwa yule mfanya biashara kutokana na kuwa busy na shughuli zake akamtumia tu hela ya kumpeleka mtoto hospital hakuweza kufika.

Yule polisi akamwambia nitakuja kesho tumpeleke mtoto hospital, na dereva wa bodaboda alimwambia atakapopata nafasi atampigia waende hospital, basi kesho yake ambayo ndio jana ikafika mchana polisi akaja wakaingia ndani akaandaliwa chakula kwanza ale ili wampeleke mtoto hospital, wakati wakiwa wote ndani mara bwana wa bodaboda naye akaja yule mama alikuwa hajui kama atakuja maana alisema atapiga simu kwanza.

Basi jamaa wa bodaboda pale si kwake na yeye ndio kufungua mlango anamkuta polisi anajivinjari misosi huku mama mtoto na mtoto wamekaa pembeni yake ndio yule mama kushtuka na kusimama ghafla kama kaona jini, akamkaribisha jamaa akaingia ndani akasalimiana vizuri tu na yule polisi bila kujuwa ni mume mwenziye mama sasa anaaza kuwewesuka mara dereva wa boda boda akaanza kumkaribisha shemeji karibu hapa ni nyumbani kwangu na hii ndio familia yangu.

Ebo!!! polisi si ndio kuanza kushangaa shemeji wewe au mimi wewe siumenikuta ndani kwangu na familia yangu halafu unasema huyo mkeo unawazimu wazimu kwa mke wangu dereva wa boda boda ndio kuanza vurugu sasa kama kawaida yao vurugu likawa vurugu mpaka kupigana ndio yule mama kumchukuwa mtoto kukimbilia kwa mjumbe.

Mjumbe kuja pale sasa watu wameshajaa ndio kutuliza lile vurugu la watu pamoja na wale wanaopigana, kuuliza kulikoni story ndio ikawa hivyo kuulizwa yule mama akasema ni kweli na wapo wa tatu kuulizwa kuhusu nani baba wa mtoto akasema wote maana alikuwa anatembea nao wote alipopata hiyo mimba!!!!!!

Basi yule polisi akasema mimi naondoka zangu na sitaki tena kusikia habari zako usinitafute kabisa, dereva wa bodaboda akasema nilikuwa najinyima nikijuwa wewe ni mke wangu na huyo ni mtoto wangu sasa sitaki tena habari na wewe mjume akamuuliza huyo wa tatu yuko wapi bahati yake alikuwa hajaja wambea wakasema apigiwe simu aambiwe kila kitu...Uswahilini bwana

Basi mjumbe na yule dada kweli wakampigia jamaa yule kaka akasema yeye ni mume wa mtu na anafamilia yake haitaji kugombania mke wala mtoto kwani anao akakata simu.

Yule mwanamke akabali pale hana lolote watu wakamzomea na kutaka kumpiga ndio mjumbe kumchukuwa kwenda naye kwake kutuliza vurugu mpaka leo hatujamuona mtaani.

Nunuu

Reactions:

0 comments:

Post a Comment