Wednesday, February 13, 2013

Uswahilini kwetu...

Wapendwa natumaini hamjambo nimewamisije sasa jamani nimerudi kutoka Arusha salama namshukuru sana MUNGU sasa nipo rasmi huku siunaelewa tena ukija unaanza kwanza kumalizia viporo ulivyoacha nyumbani haswa chumbani na ubavu wako ndio hayo yaliyonibana mpaka jana leo ubavu wangu umesafiri na hivi nipo likizo basi nimeona ni muda muafaka wa kukaa hapa niwape mbili tatu zilizotokea mtaani kwetu.

Kwanza nimerudi nikakuta mtaani kwetu kuna misiba miwili na kituko kimoja ambavyo najuwa kwa namna moja ama nyingine vitawasaidia sana humu kuna baba mmoja alikuwa ameoa na wamekaa kwenye ndoa yao miaka mingi tu na kubarikiwa kupata watoto wawili ambaye mmoja yupo boarding na mwengine yupo tu nyumbani.

Jamani wanaume kila siku mimi nasema usipotubu dhambi yako ya kumsaliti mkeo na kupenda mahawara siku moja kabla ujauonja umauti utailipia hata kama itakusababisha kupoteza maisha lakini utailipa dhambi yako hiyo.

Huyu baba japo alikuwa ameoa alikuwa na hawara ambaye alikuwa ni mama mtu mzima na mwenye hela zake nyingi sana mkewe hakujuwa lolote kuhusu huyu hawara kumbe ndiye laiyekuwa anamweka mumewe mjini kwanzia gari mpaka biashara zake na hata hela za matumizi ya nyumbani yote hawara anahudumia.

Maisha yalienda hivyo miaka mingi mpaka yule baba akanogewa na kwenda kumtambulisha yule hawara kwa wazazi wake mbeya kijijini wakawa wanamjuwa na kwa vile alikuwa na hela basi alikuwa anawahudumia sana wale wakwe hata la kusema wakwe walikuwa hawana mbele ya mkwe wao huyo, na hawakujali tena kama jamaa alikuwa mume wa mtu bali waliweka pesa mbele.

Miezi mitatu iliyopita yule bwana alisafiri kwenda musoma kibiashara alikaa huko hiyo miezi mitatu, mara yule hawara yake akamuita arudi dar ya kwamba amemnunulia gari ndogo ya biashara kwahiyo alika aitest basi bwana mwenyewe kwa furaha tele ndio kurudi siku ya alhamisi kulala kwake asubuhi na mapema bila hata kumuaga mkewe akaondoka mpaka kwa hawara yake kwenda kuchukuwa ile gari.

Walichokifanya huko wanajuwa basi mida ya mchana ndio jamaa kuchukuwa ile gari na rafiki yake mwengine kwenda kuitest hata mbali hawakufika wakapata ajali mbaya yule mume wa mtu akafa hapohapo dereva yeye alichubuka tu!!!!!!

Taarifa zikamfikia mke mtu kama kawaida sisis tunazimia mara mia tunalia sana tukililia wame zetu tuliowapenda leo wametuacha, basi taratibu za msiba zikafanyika na wakaamua kwenda kuzika mbeya nyumbani kwa yule baba, ndugu zangu na kule hawara kaenda siku moja kabla maiti haijafika kwenye maziko yupo karibu na wazazi utamwambia nini..chezea pesa weye

Watu wakafika na taratibu za mazishi zikaanza kesho yake kwakuwa watu wengine hawakumjua shoga ambaye alikuwa karibu sana na wazazi wakaanza kumshangaa lakini yule dereva yeye alikuwa anamjuwa ndio kusema ile gari maerehemu alipewa na huyo bidada kwamba ni hawara yake, msiba sasa ukageuka kuwa ngumi mke mtu acha apigane kashasahau kwamba wanayempigania kalala hajitambui.

Mara ndio watu kuwakalisha chini na kuwasihi wamzike yule baba salama na baadaye wajue kisa kizima ndio yule hawara kuhadithia kila kitu mpaka kijijini wanamjuwa na hela zote anazotesea mumeo mimi ndio nilikuwa nampa, yule dereva akasema hawa walikuwa wote siku nyingi lakini huyu mama watu wanamjuwa ndio zake kula serengeti boys na kila hawara anayekuwa naye anakufa, ni kama anatolewa kafara.

Tulimwambia mwenzetu baada na sisi kupewa hizo taarifa na mtu aliyekuwa anamjuwahuyu mama lakini yeye hakutuamini na kutusemea kwa mama na kila mara kutokea ugomvi mkubwa, mpaka yalipomkuta haya.

Watu ndio kuanza gumzo pale na kumfukuza yule mama na kuendelea na msiba wao ambao uliisha juzi.

Kweli dunia imefika mwisho utajiri sasa hivi ndio mpka kutoa wame za watu kafara!!!!! akianani

0 comments:

Post a Comment