Jamani uuuwwiii nilikuwa nasikiaga story za waganga ila jana ndio nimejionea kwa uwazi, hivi binadamu ukifanikiwa tabu, ukioa na kuolewa tabu yani mtu mmoja analogwa na watu watano hivi unategemea nini jamani si mtoto wa watu atachanganyikiwa mkewe amloge, wapangaji wake wamloge, mahawara wamloge, kazini wamloge huyohuyo mtu mmmoja tena kwenye mahawara kama ndio anao zaidi ya watatu wawili watakuwa wanamloga sasa huyo mtu anakuwaje??????? anyways back to my point
Jana mida ya saa kumi na mbili jioni nikiwa nyumbani nikasikia makelele aya watu wakisema mtoemtoe shoga yako sasa nilivyokuwa mwingi wa habari nipate kuwaletea humu nikaenda kama kawaida yangu yani mambo ya mtaani lazima yanifikie katika kiti changu cha juu, kufika pale watu wanazozana kwamba kuna nyumba moja ya baba mmoja hivi ameipangisha kwamba wapangaji wake wanamloga ndivyo alivyotonywa na mtu.
Basi yule baba alivyoyajuwa hayo akaamua kwenda kwa mganga ili aje atoe huo uchawi ndio mganga akawa amekuja sasa anafanya madawa yake huko na kule ongea hili na lile mara baada ya muda ukatokea mshtuko tu halafu kitu kikapanda juu yani nilitaka kuzimia kama vile kwenye movie za kinigeria basi likatika kitu kama jiwe jeusi limefungwa na kitambaa yule mganga akalichukuwa akamwambia yule baba mwenye nyumba avue nguo avae kitambaa chekundu cha mganga kweli yule baba akafanya hivyo.
Kumbukeni hapo tupo nje ya nyumba yake na watu wamejaa kibao na wapangaji wake pia wamo basi baba kufwata masharti ya mganga akavua nguo mbele ya watu na kuvaa kitambaa cheupe akakabidhiwa ule mzigo baada ya yule baba kuupokea yani pakawa kama panamvutano lile jiwe kama linataka kupeperuka basi akawa analing'ang'ania sana kwa nguvu akaambiwa na mganga akikisha lisikudondoke ama madhara yake yatakuwa makubwa sana akaling'ang'ania mpaka ile nguvu ya mvutano ulipoisha ndio akamkabidhi yule mganga.
Palipotulia watu wakamuuliza mganga kwani humo ndani palikuwa na nini akasema mule ndani palikuwa na viungo vyote vya yule baba kwanzia kichwa mpaka miguu hee watu ndio kushangaa mbona vitu vyake anavyomwenyewe mganga akamuuliza yule baba unamuda gani tokea ukutane kimwili na mkeo yule baba akasema kama mwaka mganga akasema mnaona maana kila kitu chake kipo humu hata uume wake ndio maana kila akifika kwa mkewe anashindwa kusimamisha na kumpa mzunguko!!!!!!!!!!!!!!huh mwaka mzima!!!!!!!!!!!
Yule baba akasema ni kweli alikuwa anajishangaa akiwa nje ya nyumba yake anakuwa mzima kabisa yani na ananguvu kabisa ya kufanya kazi lakini akirudi nyumbani tu anakuwa amechoka yani hawezi kufanya kitu chochite zaidi ya kula na kulala kwa mwaka mzima hiyo hali ilimtokea akasema hakuwa hata na hamu ya kukutana kimwili na mkewe kabisa.
Basi mganga akatengeneza dawa na kila mtu anayekaa kwenye hiyo nyumba akaambiwa aoge hiyo dawa kila mtu akaioga mganga akakusanya vitu vyake na kuondoka na kutuachia gumzo mtaani.
Hivi kwanini binadamu ukamloge mtu ili iwaje halafu na baada ya hapo ikusaidie nini, MUNGU ndiye muumbaji na yeye tu ndio mwenye kukupa na kukunyang'anya kitu kama unahisi unahitaji kitu labda hukukipata kwasababu sio chako na hustahili lakini kama unastahili basi atakupa maana si alisema kila aombaye atapewa, atafutaye ataona na abishaye atafunguliwa na pia yeye hujibu kwa wakati wake kama unaona umeomba sana na hujajibiwa umechoka basi juwa hicho sio chako katafute chako, usizidi kupoteza wakati wako na kujitia nuksi.
0 comments:
Post a Comment