Monday, January 28, 2013

Wanandoa....

Leo nataka niongee na wanandoa najuwa kabla hamjaoana huwa wengi huficha makucha yao haswa katika tabia zao, lakini jamani kuna vitu na vitu vya kuficha hakuna kitu kibaya kuficha kama kazi yako unayoifanya ya kukupa kipato, yani katika vitu muhimu hicho usiwahi kumficha mwenzio kwasababu kinaweza kuleta matatizo sana huko mbele namaanisha nini sikia kisa hiki..

Uswahilini kwetu kuna wanandoa ambao wameoana mwezi sasa, kumbe katika ndoa yao klikuwa kuna matatizo ya chini kwa chini nyumba hiyo hawajawahi kula nyama hata siku moja yule mke akajuwa labda ni matatizo ya kifedha yanayomkabili mumewe akawa anamvumilia siku zinazidi kwenda mama anadai amechoka kula hizo mboga nyengine anataka kula nyama yule mumewe akawa anamwambia hataki nyama ipikwe nyumbani kwake bila kutoa sababu ya maana.

Siku hiyo yule mwanamke akamkalisha mumewe chini na kumuuliza kwa nini hataki ale nyama mule ndani yani kila akitaka nyama mpaka akale kwa ndugu zake na labda akale barabarani mumewe akawa sasa ameshachoka na zile kero akamwambia mkewe kwamba kwasababu unataka nyama basi leo nitakuletea nyama, yule mama akamshukuru mumewe na akwa na furaha kweli ya kwamba kwa mara ya kwanza atapika nyama nyumbani kwake.

Yule baba akaenda kazini jioni aliporudi akarudi na mfuko wa nyama mkewe alikuwa chumbani wakati anaingia akaitoa ile nyama akaiweka mezani na kumuita mkewe mkewe akaja kwa furaha kumpokea mumewe lakini alipofika alipo mumewe alidondoka kwa mshtuko kwa kuona kitoto kilichokufa mezani kwake.

Akaanza kupiga kelele kwa nguvu majirani ndio kuja na kuanza kushangaa na wao yule mumewe akamwambia kila siku mke wangu nakwambia usipike nyama humu ndani sikutaka kukuambia kwa nini ila nilitegemea kama mumeo ungenielewa acha leo ujuwe kazi yangu mimi ni ya kuosha maiti na huwa sipendi kabisa kula nyama kwasababu kila siku na zishika siwezi tu kula nyama.

Basi tena pale watu ndio kuanza kushangaa na yule mama ndio kuanza kulia hakujuwa kama mumewe kazi yake ilikuwa kuosha maiti basi majirani ndio kuondoka yule baba kuchukuwa kile kitoto na kukipeleka sijui wapi kwanzia hapo naona mkewe hatodai nyama tena kwa mumewe.

Tusifichane vitu jamani kama kakupenda kakupenda tu na kama atakukimbia basi hakukupenda kwa dhati

Reactions:

3 comments: