9:43 PM
Shalom
Jambo hili limezua migongano mingi sana kwenye ndoa hadi kupelekea
ndugu kuona kwamba mke au mume anamzuia ndugu yao kuwasaidia. Pia
imeleta shida kwa wanandoa wenyewe kwa wenyewe. Tatizo maranyingi sio
ndugu bali ni wanandoa, mmoja anapoamua kutoa msaada kwa ndugu wa upande
wake bila kumshirikisha mwenzie.
Mume na mke ni mwili mmoja,
haijalishi nani anakipato kikubwa, nani anafanya kazi au familia ipi
inauhitaji mkubwa; haitakiwi na si sawa kwa mwanandoa mmoja kuwasaidia
ndugu wa upande wake kimya kimya. Hili ni kosa ambalo limewagharimu
wengi, mwenzio akigundua kuwa unasaidia ndugu zako hata kama ni kidogo
kiasi gani bila kumshirikisha hatafurahia, ataumia kwa nini umemficha na
atajiuliza ni mangapi mengine unamficha.
Usitoe chochote nje ya familia bila kumshirikisha mwenzi wako, kabla
hujaamua kumsaidia mshirikishe mwenzi wako na kwa pamoja muamue msaada
gani amtatoa na kwa kiwango gani na kwa muda gani. Pia kama mmeongea
ikaonekana hamna uwezo wa kutoa msaada kwa wakati huo, usiende kusema
mimi ningekusaidia lakini mwenzangu kakataa”,kwenye ndoa hakuna mimi na
yeye bali wote ni mmoja hivyo mweleze hali hairuhusu kwa wakati huo.
Pia usimkaribishe ndugu kuja kuishi nanyi bila kuongea kwanza na mwenzi
wako na mkakubaliana katika jambo hilo. Ni rahisi ndugu kusema
nanyanyasika kumbe mwanandoa mmoja amechukua maamuzi ya peke yake na
hivyo huyu aliyepuuzwa anamalizia machungu na hasira kwa ndugu
aliyekuja. Matatizo mengi katika ndoa yatamalizwa kwa ushirikishwaji wa
kina kwa wanandoa wote na kutokufanya jambo lolote bila kumshirikisha
mwenzi wako.
Source: Women of Christ
0 comments:
Post a Comment