Wednesday, January 30, 2013

Lalamiko kuu la wanaume...

Katika pitapita zangu za mtaa nikakutana na wanaume wamekaa wanaongea mambo ya uhusiano na wanawake zao lakini katika kundi hilohilo kunwa wanaume ambao hawana wanawake na labda hawajaoa kabisa walikuwa wanazungumzia maisha ambayo wanatarajia siku wakio wawe nayo halafu wakaongelea kitu kimoja ambacho wote waliokuwepo hapo wakawa wanakubaliana nalo kuhusu wanawake kwamba mwanamke siku zote ikija kwenye pesa changu "chake chake chake mwenyewe".

Kuna kitu nataka wanaume watambue unapozaliwa na kujitambua kuwa wewe ni mwanaume basi akikisha unakula kwa jasho maisha yako yote ujitume katika kufanya kazi uhakikishe siku unapoamua kuoa unakipato cha kuendeleza familia, hata vitabu vya dini vimeandika kwamba baba ndio kichwa na muhudumu katika familia yani wewe unapotaka kuoa ujuwe ni jukumu lako kuhudumia nyumba yako labda tu mkeo atakapoamua kukusaidia ndio akusaidie kutokana na maisha kwa sasa yalivyo magumu lakini sio wewe kumsema na kumlazimisha ahudumie nyumbani nusu kwa nusu na wewe hapana.

Na pia wanawake wengi hupenda sana kusaidia wame zao lakini hawafanyi hivyo kutokana na majibu wanayopata kutoka kwa wame zao kwa mfano kuna dada mmoja mumewe alikuwa anajenga nyumba yao ikafika wakati mumewe akakwama basi yule dada akajitolea kufanya vitu vingi sana kwenye hiyo nyumba yao lakini kuna siku yule baba akagombana na mkewe na kumfukuza kama mbwa mke alipomuuliza mumewe kwanini anamfukuza kwenye nyumba aliyomsaidia kujenga mume akamjibu kwani nilikuomba siulifanya mwenyewe!!!!! kweli kwa namna hii unategemea mwanamke atakuwa na moyo wa kusaidia kitu nyumbani????

Wanaume nyie ndio mnaosababisha wake zenu kutowasaidia na kutotumia hela zao nyumbani mkeo anapokufanyia kitu kuwa na moyo wa shukrani na usituumie uwanaume wako kumnyanyasa kisa unajuwa mali ni yako, wanawake sisi tunaridhika na vitu vidogo mumeo anapokusifia kwa kufanya kitu basi unampa moyo wa kufanya zaidi na zaidi na hapo ndipo maendeleo yanapokuja na baraka kuzidishiwa kwenu.

Tujifunze kwa hili.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment