Thursday, December 27, 2012

Uuuwwiiii...Naumwa

Wapendwa natumaini wote ni wazima naandika hii post leo nikiwa namaumivu sana mwanzo wa mwaka niligundua ninaukama mauvimbe kwenye ziwa langu la kushoto mama yangu akaniwekea appointment Ocean road nikaenda kuangaliwa kweli wakagundua kuna kama mauvimbe wakaniuliza kama bado nilikuwa nanyonyesha nikawaambia nilishamuachisha mwanangu wakanishauri niende Agakhan kufanya Ultrasound ya maziwa nikafanya wakasema hakukuwa natatizo lolote nikarudisha report Ocean road wakaniambia hakukuwa na tatizo lolote.

Sasa wiki mbili zilizopita nikaanza tena kusikia maumivu upande huohuo wa kushoto sasa mpaka mkono wa kushoto wote unauma nikijicheki mwenyewe bado naona kuna mauvimbe jumamosi iliyopita nikaenda kwa doctor wangu Agakhan akaniambia kesho nikafanye tena Ultrasound waangalie nikamuuliza kwani kama ni cancer inakuwaje akaniambia inakuwa inavimba na ugumu kama mfupa..

Leo nilivyoamka nikajishauri ngoja nijipime tena nikajipima nikagundua sasa kumevimba kitu kama kigumu au sijui ndio uoga ninahisi tu kukibonyeza kile kitu kama ndio nimetonesha ugonjwa yaani mkono wa kushoto unaniuma jamani sijapata kuona yani ninamaumivu hapa ndio najiandaa nirudi hospital kwahiyo leo sitapost kitu chochote wapendwa ila nitakapojisikia vizuri nitajitahidi kupost hata kwa mkono mmoja.

Ahsanteni na nawatakia weekend njema.

Reactions:

4 comments:

  1. Natumai itakuwa sawa. God be with you

    ReplyDelete
  2. Ugua pole, nakutakia nafuu ya haraka. Pole kwa maumivu mwenyezi Mungu akuafue.

    ReplyDelete
  3. Ni wewe Da Rose? Pole sana. Haitakuwa cancer huwa kuna uvimbe tu hutokea dada

    ReplyDelete