Monday, December 17, 2012

Msaada Tutani...

Dada Rose, na wote mnaoingia humu mimi ni mwanaume nimeoa na ndoa yangu inamiaka sita sasa mimi na mke wangu tumebarikiwa kupata watoto wawili wakike na wakiume, ninamiezi miwili sasa dada naishi nikiwa sijielewi nimeona nikuandikie hapa pamoja na wengine mnipe ushauri nini cha kufanya. Miezi miwili iliyopita siku moja mke wangu alilalamika anaumwa na kweli alikuwa sio wa kawaida anatapika na kuishiwa nguvu kabisa ikafikia mpaka akawa anapungua sana kila nikimshauri alikuwa ananiambia ningoje ataenda tu hospital akizidi kujisikia vibaya na kweli kunasiku mpaka akashisi kuzimia ndipo aliponiambia nimpeleke hospital. Tulipofika akapimwa malaria na typhoid akawa hana lakini akawa anaishiwa nguvu ikabidi wamlaze ili wamfanyie uchunguzi zaidi baada ya uchunguzi doctoa akaniita asubuhi niliyoenda kumuona mke wangu na kuniambia anamazungumzo nami ndipo aliponiambia mke wangu alikuwa ameathirika ana ukimwi. Rose sitakaa kusahau nilipoyasikia hayo maneno niliishiwa nguvu,nikataka kupiga makelele lakini doctor aliniambia nichukuwe taarifa hizo kijasiri. nilikuwa sijui ni namna gani nitaenda kuongea na mke wangu na pia nikawa nashauku ya kujuwa afya yangu maana kama mke wangu ameathirika basi na mimi nitakuwa nimeathirika tutawaachaje watoto na bado wadogo, sikumwambia kitu mke wangu siku hiyo nikaamua kwenda nami kupima chakushangaza sikuwa nimeambukizwa sikuamini nikarudi kwa yule doctor akaniambia hilo linawezekana kwamba nisubiri tena miezi mitatu ndio nipime. mke wangu sasa alianza kupata nafuu ndipo yule doctor na mimi tukakaa naye siku hiyo na kumueleza ukweli kuhusu afya yake lakini hatukumwambia kama mimi nilipima nikawa sina. alipatwa na mshangao na huzuni akawa kama anataka kuzimia akapewa husia wa kuishi na huo ugonjwa na vitu vya kula pamoja na kuanza kutumia dawa siku hiyo tukaruhusiwa kuondoka kurudi nyumbani. ni mwezi wa pili huu sasa sijamgusa mke wangu, sijamwambia kama nimepima sina maambukizi, hatujaongea amepataje na alikuwa na husiano na nani yani sijielewi nini cha kufanya Rose nipo tu nahisi kuchanganyikiwa sijui jinsi ya kuongea ili nisiwe na jazba sijui kwakweli naombeni mnisaidie.

Victor

5 comments:

  1. Victor,
    Najuwa nimagumu sana unayopitia kwa sasa lakini kwa ushauri wangu mimi sioni sababu ya wewe kumuacha mkeo au hata kutengana naye chumba, naamini ulipomuoa ulimuoa kwenye shida na raha raha mlipata na hiyo ni moja ya shida nyingi zilizopo kwenye ndoa, amepataje huo ugonjwa labda kweli alikuwa na uhusiano nje na hakuwa makini lakini sio wakati wa kumlaumu ama kumuonyesha dharau maana kuna sababu nyingi ambazo labda zilimpelekea kutoka nje ya ndoa ni nyie tu mnazozijuwa, na labda hata wewe pia unatoka nje ya ndoa sema umekuwa makini hukupata maambukizi jiulize ingelikuwa wewe mkeo angekuacha??? maana naamini ni wewe tu ndio unamjuwa mkeo vizuri nenda mkapate ushauri kwa watu wanaotoa ushauri wa mambo ya ukimwi, rudi nyumbani ishi na mkeo siku hizi dawa zipo na ukila vizuri utaishi maisha marefu sana na yenye afya. usimuache mkeo wala usimtenge utamsababishia apoteze maisha kabla ya wakati wake muda huu anahitaji upendo haswa kutoka kwako mumewe.

    ReplyDelete
  2. mie nakusihi kaka angu,tafuta watu wazima wenye uelewa na ambao wako karibu na nyie mkae kikao mliongee na pia ajijue kma anahuo ugonjwa ili uweze kupata aman na yy hapate aman maisha yaendelee ila usimuhache mkeo na ktk kujamiana muwe mnattumia kinga mna hatakuwa ashajijua na pia hatafarjika sana akiona bd unampenda na zidisha mapenzi mara mia ya mwazo.

    ReplyDelete
  3. KAKA VICTOR HUYO NI NYOKA ABAKI KUWA MZAZI MWENZO TU

    ReplyDelete
  4. Vp watoto nao jamani? Nenda check na wanao ujue mustakabali mapema na jinsi ya kuwasaidia kuishi kwa tahadhari na mama yao ili wasijepata maambukizi km hawajayapata.

    Ningumu sna kukabiliana na hali hiyo hasa ukijiona wewe uko salama na mwenzako ameathirika, Me sioni kama utaweza tena shiriki nae tendo la ndoa ni ngumu we mueleze ukweli kwamba wewe huna na unamjali kama mkeo ila hilo tendo hapana na ni kwa manufaa ya watoto msijekufa wote bure mkawaacha watoto yatima mapema

    ReplyDelete
  5. Kaka victor ni Vyema mkaenda kupima ili muweke mambo wazi ili aweze kuishi kwa matumaini. Mshauri amrudie mungu wake kwani hakuna Ugonjwa mungu hauponi. Inawezekana pia maambukizi hakuyapata kwenye Uasherati inawezekana aliuguza mgonjwa au alichomwa na kitu. Suala ni kumwomba mungu akupe hekima, busara na upendo ili uweze kuitazama familia yako.

    ReplyDelete