Sunday, December 16, 2012

Aaaahhhhh Mama Mkwe wee....

Natumaini wote humu ndani ni wazima jamani, weekend ilikuwaje majumbani wote wazima namshukuru MUNGU kama kila kitu kwenu ni sawa hata mimi kwangu kila kitu ni safi kabisa.

Leo jamani nataka niongelee swala la mama wakwe na hii iwaendee wote mliokwenye ndoa na mnaotaka kuingia kwenye ndoa haswa wanawake, jamani kuna wanawake wengine vichefuchefu yani jamani kisa yeye kaolewa na huyo mumewe anajiona yeye ndio yeye mumewe amsikilize yeye na wengine wanakataza hata wame zao kuwa na ukaribu na mama zao kama zamani.

Kumbuka ni huyuhuyu mama ndio aliymbeba huyo mumeo miezi tisa tumboni, alipomzaa hakulala kwa amani wiki ya kwanza kabla kitovu kudondoka anakesha ahakikishe kitovu kisidondokee umeni kijana akaja kukosa nguvu za kukupa wewe raha, akamtunza mpaka akasoma akakuwa kijana akalishwa kapendeza ndio ukamuona na kumpenda wewe sasa kwanini wewe usimpende mama mkwe wako..INAHUSU

Tena utamkuta mwanamke anampiga kikumbo mama mkwe wake na maneno kibao akija kuwatembelea nyumbani jamani hata MUNGU hapendi hebu tujaribu kuwapenda hawa wamama tuone kama ndoa zetu hazitakuwa na baraka na amani tele.

Natambua kuna wa mama wengine wanagubu tena kubwa lakini akifanya gubu jitahidi kumpenda na kumuheshimu usitukanane naye na kumfanyia vituko kama mke mwenzio haipendei kabisa..

Sikukuu ndio hiyo yaja hebu mnunulie mama mkwe wako hata tenge la wax bubu kama huwezi kumnunulia wax jifanye tu umempelekea zawadi uone kama hatafurahi na umshukuru kwa kuwa mama mkwe wako na kukupa mumeo, shukrani watafurahia na kujiona ni wamuhimu sana katika maisha yenu.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment