Monday, December 17, 2012

Kitanda cha NDOA....

Jamani wanandoa hivi kitanda chako unakijuwa vizuri? haswa wanaume ama kwa vile sio jukumu lako kutandika na kununua mashuka hujui kabisa kitanda chako kipo vipi wewe ukija umechoka ulale ukitaka mzunguko ukitumie lakini hukijui kabisa.. unajuwa ni godoro gani zuri kulalia unajuwa ni mbao gani murua ngumu za kitanda cha ndoa, mashuka je unajuwa kama kunamashuka yana maana yakiwa kitandani..hehe heiya ndio maana mwakani MUNGU akipenda nataka nifunde wanaume na wanawake kwa pamoja ili mengi myajuwe.

Sharti kuu la kitanda cha ndoa lazima ulale bila nguo yani mtupu kama ulivyozaliwa kwa waliofundwa haya wanayajuwa lakini kwakuwa ndoa za siku hizi tunazichukulia poapoa tu wanawake hawataki kabisa kufundwa kabla hawajaolewa wanafanya tu wanavyojuwa wao na wayaoangalia kwenye tv wakidhani hayo ndio maisha wakati mwanamke mweusi wa kiafrica unatofauti nyingi na mahaba tele unayotakiwa kuyafanya chumbani ukijitambua.

Kitanda cha ndoa unatakiwa ulale bila nguo labda kwa heshima ya watoto kama wale wangu ambao wao chumba cha baba na mama ni kama chao ndio unavaa kitenge ukijifunika ili hata wakiingia ghafla umesahau kufunda mlango wasione walipotokea lakini ikifika wakati wa kulala chumba kikiwa kimefungwa kitenge tupa huko.

Kitanda cha ndoa mwiko kulala mzungu wa nne, yani wanandoa mimi nashangaa unalala na mumeo mzungu wa nne halafu iweje nitaandika mada kuhusu madhara ya mzungu wa nne, unatakiwa kile kitanda mlale hata kama hamuongei mmegombana lala tu wote mmegeukia upande mmoja hata kama hamtashikana usiku kucha lakini usiruhusu kulala mzungu wa nne kwenye kitanda chako cha ndoa.

Wanawake wengi wanapoolewa hata mimi nikiwa mmoja wapo unapewa godoro, unalijuwa maana yake ya kwamba umeshakuwa nenda kaanze nyumba yako na wewe ukifika sio lile godoro kisa mnachumba cha wageni ndio ukalipeleke kule hapana, lile godoro unatakiwa mlalie nyie, kama umeolewa na mumeo alikuwa anagodoro lake utalitoa na kupeleka chumba cha wageni halafu lile ulilopewa ndio utandike kwenye kitanda chenu mlalie hiyo ndio maana ya lile godoro yani mmeanza upya katika kila kitu mpaka kulala.

Kama ulikuwa hulijui chukua hilo...




1 comments:

  1. Jamani mimi godoro na kitanda vilikua vidogo nikanunua kikubwa na godoro kubwaa sasa nimeharibu?

    ReplyDelete