Tuesday, November 20, 2012

Hili jiji Nomaaaaaa...yani Bayaaaaa

Kuna dada mmoja anasoma chuo buguruni na pia ni mfanyakazi hivyo jioni akitoka kazini ndipo huenda shule.Sasa akiwa njiani kuelekea chuo akapigiwa simu na

mtu asiyemfahamu akajitambulisha kwamba yeye ni daktari wa lugaro hosp na

kumuulizia habari za mwanae ambae alishawahi kwenda kumtibu pale chakushangaza zaidi akataja mpaka aina na rangi ya nguo aliyovaa siku ile alipokwenda hapo hospitali na yote yalikuwa kweli. Na zaidi akamwambia najua sasa hivi unaelekea chuo buguruni na kweli ilikuwa hivyo, lakini mwishoni akamweleza kwamba kuna mambo anataka kujua kujua kuhusu hicho chuo hivyo na anaelekea huko hivyo akifika tu atamtafuta. Kwa muda wote huo huyo dada hakuweza kabisa

kumkumbuka ila akajipa moyo kwamba yamkini huyo mtu atakuwa anamfahamu vizuri. Baada ya kutoka chuo akiwa na wenzake watatu akawa anawasimulia habari za huyo mtu ndipo simu yake ikaita,kupokea yule mtu akamwambia nakuona uko na wenzio wawili mnavuka barabara na kumueleza jinsi alivyovaa sasa wenzie wakasema

huyo mtu anakufahamu haiwezekani hapa tupo watatu kweli na ameweza kukutambua. Kisha huyo mtu akamwelekeza mahali alipo ambapo haikuwa mbali na barabara. Lakini alipomtazama hakumfahamu kabisa, basi akampa mkono kumsalimia,

baada ya hapo hakujitambua na zaidi alijikuta yuko maeneo ya chuo kikuu cha DSM akiwa hoi. Kuangalia simu na kila kitu chake kilikuwa salama na hakufanyiwa kitu chochote, kwa bahati kulikuwa kuna ndugu yake anasoma chuo hivyo akawasiliana nae ili kupatamsaada ikabidi awahishwe mwananyamala hosp lakini kaonekana sumu iliyotumika ni kali na dawa yake wanayo regency hosp,hivyo akawahishwa regency na kupata matibabu. Baada ya ufahamu kumrudia akakuta mtu huyo kachukua pesa

zote kwenye mpesa,tigo pesa na bank (NMB na CRDB) kiasi cha milioni 3, hivyo inawezekana walipompa sumu alitaja password pasipo kujijua. Na bank walipotazama kwenye ATM Camera waliona picha ya huyo mtu na yeye alimkumbuka vizuri, lakini polisi Kijitonyama wakakiri kwamba kesi hizo sasa hivi zimetokea mara nyingi na

huo mtandao ni mkubwa, walipoenda kwenye usajili wa simu walikuta ni huyo huyo na

jina lake ndilo alilojitambulis ha.Ingawa polisi wameshindwa kumkamata.

Akiwa kituo cha polisi mara huyo mtu akampigia simu akimwambia ‘’kumbe wewe ni muoga sana tutakurudishia pesa zako’’. Sasa kumbe wanachofanya wanakuambia’’ tutafutie mtu ambae unahisi ana pesa kuliko hizi halafu tukifanikiwa tutarudisha pesa zako’’ hivyo inawezekana nae kuna mtu anaemjua alifanyiwa hivyo akaamua kumtaja yeye. HIVYO NI KUOMBA MUNGU NA KUWA WAANGALIFU

0 comments:

Post a Comment