Thursday, November 1, 2012

Gubu la Mawifi...

Eenhhee ndio jamani hii ni kwa mawifi wote, kama unajuwa wewe unakaka hii inakuhusu mimi nashangaa jamani mawifi kisa cha kumtesa mtoto wa watu ni nini kisa mmemuoa, milimtoa kwao kwa vifijo na vigelegele sasa yupo kwenu mnampigia kelele.

Jamani kuna dada mmoja ameolewa jumosi iliyopita, jumamosi tu hana hata mwezi sasa mumewe yeye anajiweza ananyumba tu kubwa yenye vyumba vitatu vya kulala shoga inaelekea hao madada wa mume hakuna aliyeolewa wote wanakaa kwao, kisa wameona kaka mtu kashaoa sasa wamejaa nyumbani kwake hta kuondoka hawataki inahusu jamani wasimuachie mdada wa watu akauzungusha nyumba nzima hivi kwanza yupo na mumewe tu wenyewe wamejazana kama nyuki juu ya mzinga.

Mawifi wenyewe afadhali basi wangekuwa wastaarabu kinachoudhi eti wakimuon kaka yao wanakuwa na adabu kaka yao akitoka wanamnyali wifi yao, eti wanaingia mpaka chumbani kwa kaka yao na kutumia vitu vya wifi yao kama mafuta, pafyum na mbaya zaidi eti pakikucha wanaenda kulala chumbani kwa kaka yao!!!!!!!! mke mtu akiwaambia kwanini wanafanya hivyo eti vitu si vya kaka yetu tutafanya tunavyotaka!!!!

Hata mwezi wa ndoa haujapita jamani, basi dada wa watu kutwa kulia hana lakufanya eti anaogopa mawifi, na hao mawifi washukuru wamepata wa kumchezea...

Wifi kama na wewe unatabia hizi shoga sio mpango huo, kunyima mtoto wa watu raha ndio nini, kujishebedua kisa kaolewa na kaka yako kama kaka yako mali siangekuoa wewe tabia mbaya haifai..LAKO hilo kama limekugusa.

Reactions:

2 comments:

  1. duh!jmn ningewapata hao wangesimulia nakwambia!hakyamungu wamepata wakumuonea uwiiiiiiiiiiiiii mie wangeshika adabu haijalishi wangeama nyumba bila kupenda mna ningewachamba mpka wangejuta.

    ReplyDelete
  2. kweli wanawake ni tatizo katika jamii,hao mawifi wanaonekana hawna kazi za kuwaingizia vipato wangekuwa na kazi wangekosa muda wakuishi kwa kaka yao hebu bi dada ongea na mumeo awaonye hao binadamu watakuharibia sasa hivi hao

    ReplyDelete