Sunday, November 25, 2012

Chezea kulea mume weye...

Kuna ndoa ilifungwa mwaka juzi 2010 na sendoff ilikuwa matata kweli, mimi kwa mara ya kwanza kuona video zikichukuliwa na makamera kama yale ya world cup ndio siku hiyo. Harusi ilifungwa kanisani lakini ukumbuni ilikuwa si kubwa sana ila nzuri tu.

 Mke wa Bwana harusi ni msomi ana degree na anafanya kazi katika moja ya taasisi za wizara ya elimu, Bwana harusi ni darasa la saba ila ni mjasiria mali. Baada ya harusi, Bwana harusi na bibi harusi walienda honeymoon kwa muda mfupi na wakarudi kuishi nyumbani kwa bibi harusi ambayo ni nyumba iliyoko kwenye taasisi anakofanyia kazi. Bwana harusi kabla ya ndoa alikuwa anaishi kwenye nyumba aliyopanga huko jijini DSM.

Baada ya mwaka mmoja wanandoa hawa wakaanza ugomvi mpaka ikafikia mahala wife akatupa mizigo ya bwana harusi nje ya nyumba wanakois

hi kule kwenye taasisi yake. Inasemekana toka wameoana bibi harusi hakuwahi kushirki tendo la harusi na bwana harusi kwa misingi kuwa anaumwa. Pia kuna wakati bwana harusi alilalamika kuwa hata bi harusi hakuwa anampa chakula anamwambia akapike mwenyewe au kama hana njaa basi ndo hivyo.

Kwa kuwarudisha nyumba uchumba wa wanandoa hawa umedumu kwa takriban miaka 13, na kuna wakati ulivunjika kwa kuwa bi harusi alikuwa amempata jamaa wa mwingine ila baadaye aliachwa na kumrudia wake wa zamani. Kabla ya ndoa kufungwa mwanaume alishauriwa na ndugu kuwa huyu mwanamke anaweza kuishi naye au kwa nini asitafute mtu mwingine, jamaa akasema kuwa anampenda na anataka kufunga naye ndoa.

Hivyo, mwaka 2011 bi harusi alienda kwa wazazi wa bwana harusi na kuwaambia kuwa hamtaki tena na amekuja kuwajulisha kuwa yeye sio mkamwana kwao tena. Mwaka jana huo huo alipata mimba na amezaa mtoto. Anapoulizwa kuwa kwa nini humtaki bwana huyu anasema kuwa hajui anachofanya na wala hatoi msaada kwa familia.

Je, kama wewe ungekuwa mshauri wa ndoa hii, ungefanya nini?

Reactions:

1 comments:

  1. kama mwanamke ana uwezo angemsaidia mumewe ili ampe kitu cha ukufanya na kuingiza ili awe productive na kama hawezi hivyo basi angemtafutia kazi au kumsomesha ili ajipatie kaajira ili waende sawa vile yeye anataka lkn mwanamke hakuwa na maarifa pia mwanaume alizidi ss alikaa tu nyumbani akimsubiri mwanamke amletee si alikuwa anata kudharauliwa na ndo yalomkuta angeomba hata msaada wakati bado mapema kabla mwanamke hajamchoka

    ReplyDelete